MWANDISHI WETU - DODOMA Utendajikazi uliotukuka wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla, umetajwa kuwa siri ya kutunukiwa Shahada mbalimbali za Heshima za Udaktari wa Falsafa kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. Akizungumzia hayo, Mbunge wa Jimbo la Pangani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, amempongeza Rais Dk. Samia kutokana na kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Nasarawa cha nchini Nigeria Aprili 11, 2026, kwa njia ya mtandao. "Rais wetu kipenzi Dk. Samia anafanya kazi kubwa za maendeleo, Watanzania, Waafrika na dunia kwa ujumla wanaziona na kuzitambua kazi zake, ndiyo maana amekuwa akitunukiwa Shahada za Heshima. Uongozi wake uliotukuka umekuwa siri ya heshima hizo anazopata," amesema Aweso. Sanjari na hilo, Aweso amesisitiza kuwa Rais Dk. Samia amejipambanua kwa maneno na kwa vitendo kuwa yeye ni mtekelezaji wa maendeleo ya wananchi ndani na nje ya Tanza...
Marato tv - Sauti ya Jamii