Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeelezea dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na wafanyabishara wadogo, wa kati na wakubwa kupitia huduma zake mbalimbali za kibenki ili kuchochea ukuaji wa uchumi na mchango wa wadau hao katika kufanikisha agenda ya Uchumi wa Buluu na uwezeshaji wa maendeleo visiwani Zanzibar. Dhamira hiyo imesisitizwa na Meneja wa benki ya NBC tawi la Zanzibar, Bw Abdul Karim Mkila wakati akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw Theobald Sabi, kwenye hafla fupi ya Uzinduzi wa Jukwaa la Kimataifa la Wakuu wa Mashirika na Kampuni visiwani Zanzibar linalofahamika kama ‘The Tanzanite CEO Roundtable, Zanzibar Chapter’ iliyofanyika visiwani humo jana jioni. Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mudrik Ramadhan Soraga aliongoza uzinduzi wa jukwaa hilo, hafla iliyohudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi, Uchumi na Uwekezaji) Zanzibar, Sharif Ali Sharif. Jukwaa hilo liliwakutanisha pamoja viongozi wa kampuni na mashirika ku...