Skip to main content

Posts

Showing posts from May 10, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mchengerwa:Pimeni afya ya akili mapema

WAZIRI wa Afya Mohamed Mchengerwa ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kupima magonjwa ya afya ya akili, hususan msongo wa mawazo na sonona, akisema changamoto hizo zinaongezeka lakini zinatibika endapo zitagundulika mapema. Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma leo Mei 11, 2026, Mchengerwa amesema Serikali inaendelea kuimarisha huduma za afya ya akili nchini ili kuwasaidia wananchi kupata matibabu na msaada wa kisaikolojia kwa wakati. “Nitoe rai kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya kupima magonjwa ya afya ya akili hususan msongo wa mawazo na sonona,” amesema Mchengerwa. Amesema kati ya Julai 2025 hadi Machi 2026, jumla ya watu 254,932 walipatiwa huduma za afya ya akili pamoja na msaada wa kisaikolojia katika vituo vya afya vya msingi nchini, huku upatikanaji wa dawa za afya ya akili ukifikia wastani wa asilimia 75 katika vituo vya kuto...

Waziri Kombo Awasilisha ujumbe Maalumu wa Rais Samia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) amewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Djibouti Mhe. Ismaïl Omar Guelleh wa nchi hiyo. Mheshimiwa Kombo amewasilisha ujumbe huo wakati wa sherehe za uapisho wa Mheshimiwa Rais Guelleh zilizofanyika Mei 09, 2026 jijini Djibouti.

Waziri Kombo ashiriki mkutano wa dharura wa kamati ya Mawaziri SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi, na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-MCO), uliofanyika  tarehe 10 Mei, 2026, Jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo uliolenga kuimarisha misingi ya amani, umeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. George Chaponda, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Malawi. Katika mazungumzo hayo, Mawaziri wamejadili  changamoto mbalimbali za kiusalama zinazoikabili kanda hiyo ikiwemo  Vurugu zinazoendelea nchini Afrika Kusini dhidi ya raia wa nchi nyingine za Afrika. Kwa Upande wake Mwenyekiti Dkt. Chaponda amewahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa mapendekezo yote yaliyofikiwa yatafanyiwa kazi kwa haraka na kwa ufanisi. Hatua hii ni sehemu ya mikakati ya SADC kuhakikisha kuwa Kanda ya Kusini mwa Afrika inasalia kuwa kisiwa cha amani, utulivu,...

Waziri Kombo ashiriki mkutano wa dharura wa kamati ya Mawaziri SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi, na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-MCO), uliofanyika  tarehe 10 Mei, 2026, Jijini Nairobi, Kenya. Mkutano huo uliolenga kuimarisha misingi ya amani, umeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. George Chaponda, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Malawi. Katika mazungumzo hayo, Mawaziri wamejadili  changamoto mbalimbali za kiusalama zinazoikabili kanda hiyo ikiwemo  Vurugu zinazoendelea nchini Afrika Kusini dhidi ya raia wa nchi nyingine za Afrika. Kwa Upande wake Mwenyekiti Dkt. Chaponda amewahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa mapendekezo yote yaliyofikiwa yatafanyiwa kazi kwa haraka na kwa ufanisi. Hatua hii ni sehemu ya mikakati ya SADC kuhakikisha kuwa Kanda ya Kusini mwa Afrika inasalia kuwa kisiwa cha amani, utulivu,...

Katambi-Serikali yaokoa Bilioni 21 Magereza

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amesema jumla ya Shilingi Bilioni 21 zimeokolewa ikiwa ni faida za Bodi ya Parole na Programu ya Huduma kwa Jamii. Ametoa kauli hiyo katika Viwanja vya Jeshi la Magereza wakati  Hafla ya Kuhitimisha Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi Namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi Namba 48 kwa mwaka 2025/2026 iliyohitimishwa na Mgeni Rasmi,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Ukonga jijini Dar es Salaam. “Tumeanza kutekeleza maelekezo yako ya Tume ya Haki Jinai ambayo wewe Mheshimiwa Rais uliiunda ili kuweza kufanya Maboresho kwa kuzingatia haki za binadamu na kuhakikisha wafungwa ambao ni wanafunzi wetu wa maadili wanapata na kutendewa haki stahiki za kibinadamu ikiwemo pia mahakama inayotembea ili kuweza kutoa hukumu kwa wakati na Mheshimiwa Rais watanzania wanakushukuru kwa kuweza kutoa msamaha kwa wafungwa 1369 ambapo umetumia kifungu cha 45 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hatua hiyo imetusaidi...

Heche aongoza Harambee ya Ujenzi wa Ofisi ya Jimbo Wilayani Bunda

 Mhe. @HecheJohn leo Aprili 10, 2026 akiwa Bunda, Mkoa wa Mara, ameongoza harambee ya ujenzi wa Ofisi ya Chama Jimbo la Bunda Mjini ambapo jumla ya shilingi milioni 15 zimepatikana. Aidha, amepokea wanachama wapya na kuwakabidhi kadi ya uanachama.

Rais Dkt.Mwinyi Aipongeza Tànzanite Queens U-20 Kwa kufuzu Kombe la dunia

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite Queens U-20, kwa kufuzu Kombe la Dunia la Wasichana U-20 litakalofanyika nchini Poland mwezi Septemba mwaka huu. Mhe. Dkt. Mwinyi amesema ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Cameroon katika mchezo uliochezwa leo tarehe 10 Mei, 2026 katika Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar, umeonesha kiwango kikubwa cha uzalendo, nidhamu na juhudi za vijana wa Tanzania katika kuipeperusha vyema bendera ya Taifa kimataifa. Amesema mafanikio hayo ni hatua kubwa kwa maendeleo ya soka la wanawake nchini na yameleta heshima kwa Taifa lote, huku akiwasisitiza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu kuendelea kufanya maandalizi mazuri kuelekea mashindano hayo ya dunia. Aidha, Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amewapongeza mashabiki na Watanzania wote kwa kuendelea kutoa hamasa kubwa kwa timu hiyo katika safari yake ya mafanikio. “Kwa niaba ya Se...

Balozi Nchimbi wateta na Mzee Makamba

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kumjulia hali, Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Yusuph Makamba katika makazi yake Tegeta Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Mei 2026.

Mtaka: Ofisi za Serikali mtuhusu watumishi kuhudhuria vikao na mafunzo

Na Marietha Kerenge -WHUSM Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka amezipongeza Wizara na Taasisi za Umma ambazo zinapeleka watumishi wake kwenye mafunzo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Amesema hayo wakati akifunga Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano Serikalini kilichohitimishwa leo Mei 10, 2026 mkoani Njombe. Mtaka ameeleza kuwa, mafunzo hayo yanasaidia kuwajengea watumishi uwezo na ujuzi wa taaluma zao husika. "Kuna viongozi hawapeleki watumishi kwenye mafunzo au vikao vya kada mbalimbali, hao watu wataongezaje ujuzi wa taaluma zao?" Alihoji Mtaka Vilevile, ametoa rai kwa waandaaji wa vikao kazi hivyo kupongeza ofisi ambazo zinafanya vizuri. Ofisi za Serikali ambazo zinapeleka watumishi wake kwenye mafunzo mbalimbali ya kada husika.

Mhe Mtaka asisitiza maafisa habari kutangaza shughuli za Serikali

Na Shamimu Nyaki -WHUSM Maafisa Habari wa Serikali wametakiwa kuongeza ufanisi katika kutangaza shughuli za Serikali huku wakizingatia mabadiliko ya teknolojia. Msisitizo huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka wakati akifunga Kikao Kazi za 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki, na Uhusiano Serikalini tarehe 10 Mei, 2026. Mhe. Mtaka amewaeleza maafisa hao kuendelea kuwa daraja kati ya Serikali na wananchi kwa kuwapatia taaarifa sahihi zinazolenga kubadilisha maisha ya wananchi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu pamoja na fursa zilizopo katika sekta ya burudani. "Mnapohudhuria vikao kazi hivi tafuteni pia fursa ambazo zitabadilisha maisha yenu binafsi nje ya kazi, tafuteni uwekezaji katika biashara, kilimo na sehemu nyingine ili kuwa na maisha bora zaidi baada ya kustaafu", ameseisitiza Mhe. Mtaka. Awali Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari -MAELEZO  aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Kelvin Kanje akimkaribisha Mkuu wa Mkoa ameeleza...