Skip to main content

Posts

Showing posts from June 22, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MWAKIOJA: UWEKEZAJI WA ZAIDI YA BILIONI 82 KATIKA MAJI WAIPELEKA MKINGA KWENYE LENGO LA ASILIMIA 100

 Mbunge wa Jimbo la Mkinga, Mhe. Twaha Said Mwakioja, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya maji wilayani Mkinga, hatua inayoweka msingi wa kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi. Akizungumza mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mhe. Mwakioja amesema wananchi wa Mkinga wana kila sababu ya kuendelea kumpongeza, kumuombea na kumuunga mkono Rais Samia kwa namna ambavyo ameendelea kuelekeza rasilimali nyingi katika miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Amesema kwa sasa upatikanaji wa maji safi na salama wilayani Mkinga umefikia asilimia 72.6, huku vijiji 67 kati ya 75 vikipata huduma hiyo. Alibainisha kuwa vijiji vinane vilivyosalia vitaunganishwa na huduma hiyo kupitia miradi ya maji yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 47 inayoendelea kutekelezwa. Mbunge huyo amesema, pamoja na miradi hiyo, Serikali imeidhinisha zaidi ya shi...

SERIKALI YARIDHIA KUTENGA ASILIMIA 10 YA MAKUSANYO YA MADINI KWAAJILI YA UTAFITI WA KINA WA RASILIMALI ZA MADINI

  Waziri wa Madini, *Mhe. Anthony Mavunde,* amesema Serikali imefikia hatua muhimu katika maendeleo ya sekta ya madini baada ya kuridhia kutenga asilimia 10 ya makusanyo yatokanayo na sekta hiyo kwa ajili ya kugharamia utafiti wa kina wa rasilimali za madini nchini. Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 Bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu Juni 22, 2026, Mavunde amesema hatua hiyo ni ya kihistoria na itawezesha Tanzania kuongeza uelewa wa kina kuhusu utajiri wa madini uliopo katika maeneo mbalimbali ya nchi. Amesema Tanzania imepiga hatua katika shughuli za utafiti wa jiolojia ambapo hadi sasa imefanya geological mapping kwa asilimia 97, geochemical survey kwa asilimia 24 na low resolution survey kwa asilimia 100 tangu tafiti hizo zilipoanza kufanyika katika miaka ya 1978 na 1979. Hata hivyo, Mavunde amebainisha kuwa maendeleo ya teknolojia na mahitaji ya sasa ya sekta ya madini yanahitaji utafiti wa kina zaidi unaojulikana kama high reso...

NCHIMBI ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA SERIKALI WA SADC ORGAN TROIKA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Serikali wa Utatu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika) kuhusu hali ya usalama nchini Madagascar na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mkutano huo, umefanyika kwa njia ya Mtandao, leo tarehe 22 Juni 2026, Makamu wa Rais akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

CHANDI MARWA AONGOZA KAMATI YA SIASA CCM MKOA WA MARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya za Tarime, Musoma na Serengeti, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa jukumu la Chama la kufuatilia maendeleo na kuhakikisha miradi ya Serikali inatekelezwa kwa ufanisi, ubora na kwa kuzingatia thamani ya fedha za umma. Akiongoza ziara hiyo leo, Juni 22, 2026, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Mhe. Patrick Chandi Marwa, amesema ukaguzi huo unalenga kujionea hatua za utekelezaji wa miradi pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazotarajiwa baada ya miradi hiyo kukamilika. Katika ziara hiyo, Kamati ilitembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, ambapo iliridhishwa na maendeleo yaliyofikiwa na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika katika Mkoa wa Mara. Aidha, imewapongeza viongozi wa Serikali, watendaji na wasimamizi wa miradi kwa usimamizi mzuri unaowezesha utekelezaji wa miradi kwa kuzingatia Ilani ya Chama Cha Mapinduz...

KAMATI YA SIASA MKOA WA MARA YAKAGUA MRADI WA MAJI WA MIJI 28 SERENGETI, YARIDHISHWA

KAMATI ya Siasa ya Mkoa wa Mara, ikiongozwa na Marwa Mathayo, leo Juni 22, 2026, imefanya ziara ya ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Chujio na Usambazaji wa Maji wa Miji 28 katika Mji wa Serengeti, wilayani Serengeti, kwa lengo la kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo muhimu unaotarajiwa kuimarisha huduma ya maji kwa maelfu ya wananchi. Akiongoza Kamati hiyo katika ukaguzi wa Mradi wa ujenzi wa chujio na usambazaji wa Maji wa Miji 28 Katika Mji wa Serengeti leo Jun 22, 2016 wilayani Serengeti  Marwa Mathayo ambapo Kamati hiyo imedai kuridhishwa na utekelezaji wa Mradi huo. kamati ilipata maelezo kuhusu hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi, unaohusisha ujenzi wa chanzo cha maji, chujio la kisasa la kusafisha maji, mtandao wa mabomba wenye urefu wa kilomita 31 pamoja na ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji lenye uwezo wa lita milioni mbili katika eneo la DDH. Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi MEGA Engineering Limited chini ya usimamizi wa Mkandarasi Mshauri WAPCOS Limi...

OFISI YA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI INAFANYA KAZI KUBWA – PROF. KAHYARARA

▪️Aipongeza Wizara ya Habari Maandalizi AFCON 2027. *Na Adelina Johnbosco - MAELEZO* Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, ameipongeza Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali na kusema inafanya kazi kubwa ya kuzitangaza shughuli zinazotekelezwa na Serikali pamoja na kuwafikia wananchi. Prof. Kahyarara amesema hayo Juni 22, 2026, alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na taasisi zake katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma. "Serikali ina shughuli nyingi zinazofanyika ikiwemo miradi mbalimbali, mipango na malengo kwa ajili ya maendeleo na maslahi ya wananchi, hata ukisema kila siku au kila wiki utoke na kitu kimoja lakini bado inakuwa haitoshi, lakini Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali inajitahidi kwa kufanya kazi kubwa kwani taarifa zinatolewa kuhusu yanayotekelezwa na Serikali kwa wananchi wake" ameongeza Prof. Kahyarara. Kwa upande mwingine, ameipongeza Wizara ya...

MWALUNENGE AENDELEA KUSUKUMA MAGEUZI YA UCHUMI MBEYA MJINI

 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Patrick Adkin Mwalunenge, anaelezwa kuendelea kuweka msukumo mkubwa katika utekelezaji wa agenda ya maendeleo na mageuzi ya uchumi kwa wananchi wa jimbo hilo kupitia mikakati mbalimbali inayolenga kukuza biashara, uwekezaji, ajira na kuboresha miundombinu ya kiuchumi. Katika kipindi kifupi tangu achaguliwe kuongoza jimbo hilo, Mwalunenge ameendelea kushirikiana na wananchi kwa kushuka katika maeneo mbalimbali kusikiliza kero zao, kubaini changamoto zinazowakabili na kuzisimamia ili zipatiwe ufumbuzi.  Hatua hiyo inalenga kuhakikisha maendeleo ya jimbo yanakwenda sambamba na mahitaji halisi ya wananchi. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ofisi ya Mbunge imejenga mfumo wa kupokea, kuchambua na kufuatilia changamoto za wananchi, huku ikielekeza nguvu katika utekelezaji wa miradi yenye tija kwa uchumi wa Mbeya Mjini na Jiji la Mbeya kwa ujumla. Miongoni mwa maeneo yanayopewa kipaumbele ni kukuza biashara za Mbeya ili ziweze kufikia masoko ya kitaifa na ki...

PRESIDENT NDAITWAH DEPARTS TANZANIA AFTER COMPLETING A THREE-DAY STATE VISIT

   The President of the Republic of Namibia, H.E. Dr. Netumbo Nandi-Ndaitwah, has departed Tanzania after successfully concluding her three-day State Visit to the country, which took place from 19 to 21 June 2026. At Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam, President Nandi-Ndaitwah was seen off by the Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Ambassador Mahmoud Thabit Kombo, alongside other government leaders, diplomats, and senior officials. During her visit, President Ndaitwah held official talks with the President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. Samia Suluhu Hassan, aimed at strengthening cooperation in various sectors, including trade, investment, education, agriculture, energy, and social development.  The two leaders also exchanged views on regional and international issues, emphasizing the importance of African solidarity in addressing development challenges and the evolving global economic landscape. President Nandi-Ndai...

PRESIDENT NDAITWAH DEPARTS TANZANIA AFTER COMPLETING A THREE-DAY STATE VISIT

 The President of the Republic of Namibia, H.E. Dr. Netumbo Nandi-Ndaitwah, has departed Tanzania after successfully concluding her three-day State Visit to the country, which took place from 19 to 21 June 2026. At Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam, President Nandi-Ndaitwah was seen off by the Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Ambassador Mahmoud Thabit Kombo, alongside other government leaders, diplomats, and senior officials. During her visit, President Ndaitwah held official talks with the President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. Samia Suluhu Hassan, aimed at strengthening cooperation in various sectors, including trade, investment, education, agriculture, energy, and social development.  The two leaders also exchanged views on regional and international issues, emphasizing the importance of African solidarity in addressing development challenges and the evolving global economic landscape. President Nandi-Ndaitwah pa...