Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesema litaendelea kutoa elimu ya kilimo bora na cha kisasa, ufugaji na uvuvi kwa wananchi hata baada ya kufungwa kwa Maonesho ya Wakulima (Nanenane), huku likiandaa mfumo maalumu wa kuwafuatilia na kuwawezesha vijana wanaohitimu mafunzo yake kujikita katika shughuli za uzalishaji na kujitegemea. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele, alipotembelea banda la JKT katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni jijini Dodoma, Agosti 4, 2026. Meja Jenerali Mabele alisema maonesho ya Nanenane ni fursa muhimu kwa JKT kuonyesha teknolojia na mbinu bora za kilimo, ufugaji na uvuvi, huku akisisitiza kuwa huduma hizo zitaendelea kutolewa hata baada ya maonesho hayo kumalizika. "Kwetu sisi maonesho haya ya Nanenane ni endelevu. Hata baada ya maonesho haya kufungwa, tutaendelea kuwepo hapa na katika kanda zote ambazo JKT linashiriki ili wananchi waendelee kupata elimu ya kili...
Marato tv - Sauti ya Jamii