Skip to main content

Posts

Showing posts from October 30, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

KAIRUKI ASISITIZA UJUMUISHWAJI WA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA MAENDELEO YA AKILI UNDE AFRIKA

Na Mwandishi Wetu, WMTH - Libreville, Gabon  Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb.), amesisitiza umuhimu wa kuwajumuisha watu wenye ulemavu katika mipango ya maendeleo ya ujuzi wa kidijitali, hususan Akili Unde (AI), ili kuhakikisha wanapata fursa sawa katika uchumi wa kidijitali. Mhe. Kairuki ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa Sita wa Kawaida wa Kamati Maalumu ya Kiufundi ya Umoja wa Afrika kuhusu Mawasiliano na TEHAMA (STC-CICT-6), unaofanyika tarehe 29–30 Oktoba 2026 jijini Libreville, Gabon. Mkutano huo wenye kaulimbiu isemayo “Africa’s Digital Future, Africa’s Voice: Advancing Innovation, Digital Inclusion and Shaping Africa’s Narrative” unalenga kuimarisha ushirikiano wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika kukuza ubunifu, ujumuishi wa kidijitali na nafasi ya Afrika katika maendeleo ya teknolojia, huku ukihimiza kuhakikisha hakuna kundi linaloachwa nyuma. Waziri Kairuki ameongeza kuwa ujumuishi huo unapaswa kuzingatiwa k...

TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

*_▪︎ Ataka viongozi wa Afrika wazingatie uwezo mkubwa walionao vijana_* _▪︎ Ashawishi matumizi ya Kiswahili kwenye mikutano ya jukwaa hilo▪︎_* WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka viongozi wa Afrika kwa umoja wao waangalie mustakabali wa vijana wa bara hilo kwa vile wana uwezo mkubwa licha ya kuwa wanakosa fursa kwenye soko la ajira. “Muhimu kwetu sote kwa pamoja ni mustakabali wa vijana wetu kutokana na uwezo mkubwa walionao. Afrika inasimama kama bara changa zaidi duniani; hata hivyo, kila mwaka, mamilioni ya vijana wa kike na wa kiume huingia kwenye soko la ajira kutafuta fursa ambazo hazipo,” alisema. “Ili kukabiliana na changamoto hii, ushirikiano wetu lazima ulenge kuwa na ubunifu wa hali ya juu. Ushirikiano katika masuala ya akili unde na teknolojia za kidijitali lazima uwe mahsusi ili tuweze kutoa mafunzo kwa kizazi kijacho cha wahandisi wa Kiafrika ambacho kitahakikisha kuwa data za Kiafrika zinasalia chini ya udhibiti wa Afrika, kwa kuzingatia Mkakati wa Umoja wa Afrika...

RAIS JOÃO LOURENÇO WA ANGOLA AHITIMISHA ZIARA YA KITAIFA, AONDOKA NCHINI

  Akiwa jijini Dodoma, Rais Lourenço alishiriki hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba pamoja na miundombinu ya barabara zake. Mheshimiwa Lourenço aliagwa rasmi na mwenyeji wake Rais Samia katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma kabla ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma Mheshimiwa Lourenço alisindikizwa na kuagwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb.) Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa Tanzania anayewakilisha Angola mwenye makazi yake Zambia Injinia Cyprian Luhemeja, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Angola Bw. Mbwana Mziray na viongozi wengine wa Serikali.

THE 153RD IPU: SAMIA'S LEADERSHIP WINS GLOBAL TRUST

 By Prosper Makene, Dodoma When 2,044 delegates from over 150 countries landed in Arusha without a single security incident, complaint or logistical failure, the world sent Tanzania a powerful message of trust — and that trust was earned by President Dr. Samia Suluhu Hassan's leadership. That was the verdict in Parliament on Monday when Mtama MP Nape Nnauye moved a special Motion to congratulate the President for the historic success of the 153rd Inter-Parliamentary Union (IPU) Assembly. The Motion was seconded by Mlalo MP Rashid Shangazi. It was a historic Assembly in every sense. The IPU was founded in 1889 and its headquarters is in Geneva, Switzerland. It is now 137 years old. In all those 137 years, Tanzania had never hosted it. The 153rd Assembly in Arusha from October 5 to 9, 2026 was the first time. It was held under a powerful theme: Enhancing good governance and empowering communities through inclusivity, trust and opportunities for all. The scale was massive. Official re...