Skip to main content

Posts

Showing posts from November 19, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mke wa Besyige amshutumu Rais Museveni kumuandaa mtoto wake kumrithi

Bi. Winnie Byanyima, mke wa kiongozi wa upinzani wa Uganda aliyekamatwa Dkt. Kizza Besigye, amemshutumu rais wa nchi hiyo mwenye umri wa miaka 81, Yoweri Museveni, kwa kumtayarisha mwanawe kumrithi. Pia alifichua kwamba mumewe, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhaini, alikamatwa kwa kusema kile alichokielezea kama urithi wa kisiasa uliopangwa. "Tunamwona akitupeleka katika mwelekeo hatari wa kumweka mwanawe, [Jenerali Muhoozi Kainerugaba] ambaye tayari amemteua kama mkuu wa jeshi, kuwa rais wetu ajaye. Na ndiyo maana naamini Dkt. Kizza Besigye yuko gerezani, kwa sababu amesema vikali dhidi ya mradi huo. Anaona ni hatari, na nakubaliana naye,". Matamshi yake yanakuja mwaka mmoja baada ya Dkt. Besigye, kiongozi maarufu wa upinzani, kukamatwa kwa utata katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Akizungumzia hali yake, Bi. Byanyima alisema kwamba Dkt. Besigye ametengwa peke yake gerezani. "Haruhusiwi kuzungumza na wafungwa wengine; hawezi kuabudu pamoja na wafungwa wengine; hawezi ...

Mradi wa majiko banifu watambulishwa Hanang

  📌 *Majiko banifu 1,583 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku*  📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku TZS 11,200* . 📍 *HANANG*  Wakazi wa Hanang waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia. Rai hiyo imetolewa  leo tarehe 19 Novemba, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mheshimiwa Almishi Hazali wakati wa uzinduzi wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika kutunza na kuhifadhi mazingira" alisema Mhe. Hazali. Mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni mwendelezo wa  juhudi za serikali  katika kutunza mazingira na kuboresha afya za  wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia. Aidha Serikali imeweke ruzuku ya asilimia 80 katik...

Makamu wa Rais Awasili Zambia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Jijini Lusaka nchini Zambia leo Novemba 19, 2025. Makamu wa Rais anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Ukarabati Mkubwa wa Reli ya TAZARA itakayofanyika tarehe 20 Novemba 2025 Jijini Lusaka. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Makamu wa Rais amepokelewa na Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Dkt. Elijah Muchima, Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Balozi, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, Maafisa waandamizi wa Jamhuri ya Zambia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoandaliwa kwa heshima yake. Pamoja na viongozi wengine, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Nchimbi ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Masanja pamoja Mkurugenzi Mku...

Waziri Mkuu Azungumza na Mawaziri, Naibu Mawaziri na Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira  na Mahusiano, Deus Sangu, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Rahma Riadh Kisuo. Kikao hicho kimefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 19, 2025.

Wakongwe Tido,Machumu kumsaidia Dkt Samia katika mawasiliano

Dodoma, 19 Novemba 2025  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuimarisha mfumo wa mawasiliano ya Serikali kwa kuteua wakongwe wawili katika tasnia ya habari kushika nafasi muhimu Ikulu. Kupitia Kiongozi kutekeleza na Ofisi ya Katibu Mkuu, Rais Samia amemteua Bw. Tido Mhando kuwa Mshauri wa Rais, Habari na Mawasiliano. Tido, ambaye ni mzoefu wa muda mrefu kwenye uongozi wa vyombo vya habari, anatarajiwa kuongea uzito na ufanisi katika kupanga, kushauri na kuratibu mawasiliano ya Serikali Kuu. Katika hatua nyingine, Bw. Bakari Steven Machumu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, akichukua nafasi ya Bi. Sharifa Bakari Nyanga, ambaye atapangiwa majukumu mengine. Machumu, anayefahamika kwa umahiri wake katika tasnia ya habari na mapato, anatarajiwa kupokea utoaji wa taarifa za Serikali na kuongea uwazi kati ya Ikulu na wananchi. Aidha, Rais Samia pia amemteua Bw. Lazaro Samuel Nyalandu kuwa Balozi, uteuzi unaolenga kuendelea kuima...

Busanda ya kumbukwa kwenye Baraza la Mawaziri la Dkt Samia

Na Mwandishi wetu  Wananchi wa  Jimbo la Busanda, wamepongeza DKT.Jafari Seif kwa kuteuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  DKT .Samia Suluhu Hassan  Mbunge wao kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Afya. Wakizungumza  kwa nyakati tofauti wamesema ni heshima ya kipekee ambayo haijawahi kutokea tangu jimbo hilo kuanzishwa Ambapo uteuzi huo umeleta faraja na matumaini mapya kwao huku wakieleza kuwa kwa mara ya kwanza Busanda imepata mwakilishi wa ngazi ya Uwaziri serikalini. Wameeleza kuwa uteuzi huo unathibitisha dhamira ya Rais  DKT.Samia Suluhu Hassan,kuhakikisha maeneo yote yanashirikishwa kikamilifu katika maendeleo ya Taifa hususani kundi la vijana. Sambamba na hilo Wakatoa ombi kwa mbuge wao awajengee    barabara ya Geita - Kahama kwa kiwango cha lami  kwani kwa kufanya hivyo itafungua fursa za kiuchumi na kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani. Pia  wakatoa kilio chao kwa Serikali ...

Mhe. Dkt Mwigulu Akutana na Mawaziri Wawili Ofisini Kwake

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Profesa Paramagamba  Kabudi pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 18, 2025