#Kukamilika kwa daraja hilo kutanufaisha Kata tano Iramba - Singida Kukamilika kwa ujenzi wa daraja la zege katika Mto Kinkungu lenye urefu wa mita 65.6 linalojengwa katika barabara ya Mtoa-Ndago Kata ya Shelui Wilayani Iramba kutanufaisha wananchi wa Kata tano Wilayani humo. Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Kamati ya Ukaguzi ya TARURA ikihitimisha Ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara mkoani Singida. Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida Mhandisi Ibrahim Kibasa ameileza Kamati hiyo kuwa Mradi wa ujenzi wa daraja hilo unalenga kuboresha mawasiliano kati ya Kata za Shelui, Mtoa, Ndago, Mtekente na Urughu na kwamba kukamilika kwa mradi huo kutachochea shughuli za maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii katika Kata hizo. "Licha ya changamoto zilizojitokeza katika hatua za utekelezaji, mradi umefikia hatua ya kuridhisha na matarajio ni kuwa utakamilika ndani ya muda uliopangwa ambao ni Septemba 15, 2025" alisema Akielezea hali ilivyokuwa hapo awali Mzee Ali Hassan Ju...
Marato tv - Sauti ya Jamii