Skip to main content

Posts

Showing posts from March 12, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji wa Miji 28 Katavi

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 13, 2026 ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Kata ya Shanwe, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi. Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 22.8 umefikia asilimia 55 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika Julai 2026. Kukamilika kwake kutasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa eneo hilo.  Baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo, Dkt. Mwigulu amemtaka mkandarasi kuhakikisha anaukamilisha kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa ili wananchi waanze kunufaika na huduma ya maji. Mradi huo unatarajiwa kuzalisha takribani lita milioni 12 za maji kwa siku.

Dkt. Mwigulu Atembelea Ofisi za Ccm Mkoa wa Katavi

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Machi 13, 2026 ametembelea Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi na kusalimiana na viongozi wa Chama hicho. Ziara hiyo imefanyika kabla ya kuanza rasmi shughuli zake za kikazi mkoani humo, ambapo anatarajiwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Zoezi la Pamoja Kati ya Jwtz na Jeshi la Marekani Lahitimishwa Msata

Na Kepteni Emanuel Ngonela Msata Pwani. Zoezi la pamoja la medani 'Justfied Accord 2026' lililohusisha Kikosi Maalumu cha JWTZ na Kikosi cha Jeshi la Marekani cha Walinzi wa Taifa Nebraska limehitimishwa tarehe 12 Machi 2026 kata ya Msata, iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani  Akifunga zoezi hilo Mkuu wa Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu ya Jeshi Meja Jenerali Said Nkambi alisema " Majeshi yetu yamejijengea heshima na uwezo mkubwa katika utekelezaji wa   majukumu. Jeshi la Marekani linaendeleza  uhusiano kwa kubadilishana uzoefu hasa mbinu za medani,  utoaji huduma tiba hali inayojenga mtazamo chanya wa wananchi kwa jeshi. Zoezi la 'Justified Accord 2026' limefanyika kwa mafanikio na maandalizi ya zoezi lijalo  yatakuwa mazuri zaidi baada ya tathmini ya zoezi kufanyika na kubaini mapungufu ambayo yamebainishwa na kufanyiwa kazi. "Marekani ni mshirika wetu wa kimkakati na tunategemea majeshi yetu yataendelea kubadilishana uzoefu katika masuala ya say...

REA YAFANYA ZIARA YA UHAMASISHAJI MIRADI YA NISHATI VIJIJINI MKOANI IRINGA* .

  📌 *Wananchi wapewa elimu matumizi bora ya nishati safi*  📌 *Wananchi wapewa elimu ya UMETA (READY BOARD* ) 📌 *REA inahamasisha wananchi kujiunga na huduma ya umeme*  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya umeme kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na matumizi ya vifaa vya kisasa vya umeme hususan majiko ya umeme ambayo yanatumia kiasi kidogo cha umeme, salama kwa afya za matumizi na kwa gharama nafuu. Hayo yamebainishwa na Wataalam wa REA waliofika mkoani Iringa wilaya ya Kilolo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa ya miradi ya REA inayotekelezwa mkoani humo. Mkutano wa mkutano na wananchi, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka REA, Abdulrazack Mkomi amesema kuwa, majiko ya umeme yanalinda afya za matumizi na gharama ni matumizi na matumizi mengine ya nishati ya mkaa na kuni. Ame kuwa, ili kuhamasisha matumizi ya matumizi safi ya kupikia, REA itaendelea kusambaza kwa wingi gesi nchini ikiwa ni sehemu ya kutangaza na kuongeza matumizi ya nisha...

Serikali imesema lishe bora mashuleni itaongeza ufaulu

DODOMA  SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kuwa ili kupata matokeo mazuri ya elimu ni lazima kuhakikisha upatikanaji wa lishe bora shuleni ili kuwajengea wanafunzi afya bora na kupata utulivu wa akili wawapo madarasani. Hatua hii inalenga kuboresha afya za wanafunzi na kuongeza ufaulu wao kitaaluma. Akizungumza leo Machi 12, 2026 Jijini Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Utoaji wa chakula Shuleni Afrika kwa mwaka huu 2026,Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidhi Ameir,Amesema lishe bora kwa wanafunzi ni msingi muhimu wa kujifunza kwa ufanisi.  Ametoa Msisitizo Kwa Wadau wa Elimu, wazazi pamoja na Jamii kwa ujumla kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula bora na maji safi wakiwa shuleni ili kuboresha afya na kuongeza ufaulu kielimu. "Wanafunzi hutumia muda mwingi wakiwa shuleni, hivyo upatikanaji wa chakula bora, maji safi na mazingira salama ya usafi ni muhimu katika kulinda afya zao na kuongez...

Dkt. Mwigulu Awasili Mkoani Katavi Kwa Ziara ya Kikazi

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 12, 2026 amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda mkoani Katavi, kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi mkoani humo. Katika ziara hiyo inayotarajiwa kuanza rasmi kesho Machi 13, 2026, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu atakagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Rais Samia Amesema Tutailinda Ngorongoro kwa Ajili ya Kizazi cha Sasa na Kijacho

 DODOMA. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro Pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea Taarifa za Tume hizo leo March 12,2026 Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma ambapo amesema kuwa Ngorongoro ni maliasili adhimu inayopaswa kulindwa Kwa manufaa ya kizazi Cha Sasa na kijacho, Kwa umuhimu wake wa kipkekee katika uhifadhi wa bioanuai,utalii,historia ya mwanzo ya mwanadamu pamoja na Utamaduni wa jamii za wakazi wa asili wa eneo hilo. Kadhalika, Rais Samia ameongeza kuwa Serikali inawajibu wa kulinda mfumo wa ikolojia unaounganisha Hifadhi ya Ngorongoro, Maeneo ya loliondo na ziwa natron ambapo amefafanua kuwa zoezi la uhamaji wa hiari lilianzishwa Kwa nia kulinda mfumo huo wa ndani ya eneo la Hifadhi wenye manufaa makubwa Kwa utalii wa nchi na urithi wa dunia....

Siasa za Ulimwengu Zinaathiri Nchi za Sadc

Hali ya sasa ya siasa za ulimwengu na vita zinazoendelea Mashariki ya kati, imesababisha madhara makubwa ulimwenguni ikiwemo kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na huo ni ujumbe tosha kwa nchi zetu kuchukua hatua Madhubuti za pamoja kujinasua. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC ambaye ni Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Ronald Lamola, wakati akifungua mkutano wa 47 wa Baraza hilo unaofanyika jijini Pretoria, Afrika Kusini Machi 12 na 13, 2026. Mhe. Lamola alisema hali hiyo inatishia mwenendo wa mnyororo wa biashara kwa  kupanda kwa gharama za mafuta duniani, suala ambalo litasababisha kupanda kwa gharama za mbolea na hatimaye bei za vyakula kuwa juu.  Hali hiyo ameitaja kama ni ya hatari kwa usalama wa chakula katika kanda ya SADC ikizingatiwa watu takribani milioni 58 wanakabiliwa na changamoto ya usalama wa chakula. Alisema kutokana na vita hivyo, kuna uwezekano mkubwa nchi za Mashariki...