WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete, ameungana na viongozi wenzake pamoja na wananchi kuhani msiba wa Mzee Hafidh Ameir Hassan, baba na mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja. Katika ziara hiyo, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipata nafasi ya kumfariji Rais Samia na familia yake kufuatia msiba huo mkubwa, huku akimwombea Mwenyezi Mungu ampe nguvu, subira na imani katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mwenza wake. Mhe. Kikwete amesema anaungana na familia pamoja na Watanzania katika kipindi hiki cha majonzi, akitoa pole kwa Rais Samia na familia yote ya marehemu. “Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.”
Marato tv - Sauti ya Jamii