Skip to main content

Posts

Showing posts from June 14, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mbunge Waitara Azishukia Kamati za Siasa Ccm Musoma Mjini na Tarime

-ATAKA WAACHIWE WANA CCM CHAGUO LAO Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara amezishukia Kamati za Siasa za Chama cha Mapinduzi ( CCM) za Wilaya ya Musoma mjini na Tarime Vijijini kuacha kuwachagulia mbunge wana CCM wanaomtaka wao. Kauli hiyo ameitoa jana juni 14,2025 kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kwaajili ya kuwashukuru wananchi kwa kumpa ushirikiano kwa miaka 5 ya uwakilishi wake. Mbele ya wanachama na wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye eneo la soka la kwa  saa nane Kata ya Mshikamano amesema yapo mambo ambayo yanafanywa na Kamati hizo za Siasa ambàyo hayapaswi kunyamaziwa. Amesema mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amefanya kazi nzuri katika utekelezaji wa ilani na anapofanya ziara ya kusoma kamati inakaa pembeni. Waitara amesema hayo mambo sio ya kunyamaziwa kuona watu wanatembea na mgombea wao mfukoni na yale mazuri yaliyofanywa na mbunge wanayabeza Amesema ana...

Mhe Mchengerwa Awataka Ma Rc, Dc Kuongoza Jogging Kwenye Maeneo yao

Na John Mapepele  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya  nchini kuwaongeza wananchi katika maeneo yao kufanya "jogging" na mazoezi ili kuimarisha afya. Mhe. Mchengerwa ametoa  maelekezo hayo leo Juni 14, 2025 mara baada ya kuongoza na kuhitimisha  mbio za pole pole (jogging) za kilomita 10 zilizoratibiwa na Wizara yake katika eneo la Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma. "Hamasa hii ya kufanya mazoezi iliasisiwa na viongozi wetu wakuu kuanzia enzi za Baba wa taifa letu Mwalimu Nyerere hadi Rais wetu wa sasa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan lengo likiwa kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa nyemelezi hivyo na sisi tuna wajibu wa kuendelea kuwahamasisha watumishi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye " amefafanua  Waziri Mchengerwa  Aidha, amewataka  watumishi wa TAMISEMI kujenga utamaduni wa  kufanya mazoezi wao pamoja na familia zao ili jamii yote ...

Dkt. Biteko Awaasa Ccm Bukombe Kudumisha Amani Kuelekea Uchaguzi Mkuu

📌 Azindua maduka ya kisasa 31 Ushirombo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,  Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewaasa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Bukombe wasikubali kuvutana na kugombana bali wadumishe amani, kuendelea kuheshimiana na kulinda utu wao hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Dkt. Biteko amesema hayo Juni 14, 2025 wilayani Bukombe, mkoani Geita mara baada ya kuzindua maduka 31 ya kisasa yaliyopo katika eneo la Ofisi za CCM wilayani humo. “Naomba niwakumbushe tena kwa sasa tunaukaribia mwezi wa Oktoba, 2025. Tunakaribia kuingia katika zoezi la Uchanguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, niwaombe tu kwamba, zoezi la uchaguzi ni zoezi la mara moja, lakini maisha yetu sisi yanadumu na yataendelea kudumu na kuna maisha baada ya kampeni na baada ya Uchanguzi. Hivyo, kwa heshima, nawaomba tuendelee kudumisha umoja, upendo na undugu uliopo bai...

Wanufaika Mikopo ya Elimu ya Juu Kuongezeka-Majaliwa

_▪️Asema Rais Dkt. Samia amedhamiria kuendelea mazingira ya Elimu ya juu._ _▪️Asisitiza Samia Scholarship pia kuwafikia wengi zaidi._ _▪️rais wa TAHLISO asisitiza Oktoba Wasomi wako tayari kuilinda amani kuelekea uchaguzi mkuu._   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa katika mwaka 2025/2026 Serikali imepanga kutoa mikopo kwa wanafunzi 252,773 wakiwemo 88,320 wa mwaka wa kwanza ili kuwafikia wanafunzi wengi zaidi. Amesema hayo leo Jumamosi (Juni 14, 2025) wakati wa maadhimisho ya miaka 21 ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu, yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma “Huu ni muendelezo wa malengo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuboresha elimu ya juu na mazingira ya wanafunzi kwa ujumla, Mwaka 2024/2025, mikopo ya shilingi bilioni 787.4 imetolewa kwa wanafunzi 248,331 ikilinganishwa na bilioni 570 kwa wanafunzi 177,925 mwaka 2021/2022 sawa na ongezeko la asilimia 40”. Kwa upande wa Ufadhili wa Samia (Samia Scholaship) Mheshimiwa ...

Balozi Nchimbi Ziarani Mkoa wa Simiyu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Ndugu Masanja Michael Lushinge (smart) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndugu Said Mtanda, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Dkt Nchimbi, alikuwa safarini kuelekea Mkoa wa Simiyu kwa ziara ya kikazi ambako anatarajiwa kushiriki kongamano la Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT).  Akiwa uwanjani hapo, Balozi Nchimbi pia alikutana na kusalimiana na Mama Janeth Magufuli, mjane wa hayati Rais John  Pombe Magufuli.