Skip to main content

Posts

Showing posts from April 12, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii
  Dk Kellen-Rose Rwakatare achangia milioni 2.2 ujenzi wa madrasa Taqwa na choo cha msikiti Mlimba Na Mwandishi Wetu, Ifakara MWENYEKITI wa Umoja wa Wazazi Mkoa wa Morogoro (UWT), Dk. Kellen-Rose Rwakatare ametoa shilingi milioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa madirisha na milango kwenye Madrasat Taqwa iliyopo msikiti wa Igima uliopo kata ya Mbingu Wilaya ya Mlimba mkoani Morogoro. Akikabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki, Dk Rwakatare aliwataka wazazi nchini kujenga tamaduni za kuwa walinzi kwa watoto kwa kuwapeleka kwenye masomo ya dini nyakati za jioni baada ya masomo ya mchana shuleni. Aidha amesema wazaazi hawapaswi kuwaacha watoto wao wakizagaa mitaani na kuwa hatarini kukumbwa na majanga mbalimbali ikiwemo ya ubakaji. Alisema madrasa au sehemu yoyote ya mafunzo ya dini ni sehemu salama kwa mtoto na yenye utulivu ambayo itasaidia mtoto kujifunza dini na maadili na kukua akiwa bora baadae mwenye kuweza kuwa hata kiongozi bora. “Nimewiwa kuja kuchangia madirisha na milango ya madrasa ...

Waziri Mkuu mgeni rasmi kongamano la Chama cha Wafadhiri Jijini Arusha

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 13, 2025 ni mgeni rasmi katika Kongamano la Chama cha Wafawidhi wa Matukio Tanzania, linalofanyika Olasiti Garden, Mkoani Arusha

Dc Kyoba awapongeza maafisa mawasiliano wa Serikali kutangaza utalii wa ndani

  DC KYOBA AWAPONGEZA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI KUTANGAZA UTALII WA NDANI Kilombero Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dustan Kyobya amekipongeza Chama cha  Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) kwa kutangaza utalii wa ndani. Mhe. Kyobya ameyasema hayo leo tarehe 12 Aprili, 2025 mara baada ya maafisa hao wa serikali kutembelea hifadhi ya Taifa ya Udzungwa. Amesema limekuwa jambo jema kwa maafisa hao wa serikali kufika katika hifadhi hiyo ya Taifa na kujionea vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo kwasababu wanayo nafasi kubwa ya kutangaza vivutio mbalimbali hapa nchini. “Nimefarijika niliposikia kundi hili kubwa linafika katika wilaya yetu  kubwa ya kimkakati kwa sababu ni wilaya inayozalisha umeme, sukari, na mpunga, pamoja na kusimamia uhifadhi. Hata hivyo amesema wilaya yake inaongoza kwa utalii kupitia hifadhi ya Taifa ya milima ya Udzungwa ambayo imezungukwa vivutio vingi ndani yake. Mheshimiwa Kyobya amesema Mhe.Rais ameridhia kutoa zaidi ya bililioni 4 ...

Mwendesha baiskeli chanzo cha kifo cha Mkurugenzi mtendaji Tanesco na dereva wake.

  MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (Tanesco), Gissima Nyamo-Hanga amefariki dunia usiku wa kuamkia Aprili 13, 2025 katika ajali ya gari iliyotokea Bunda mkoani Mara. Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Mtambi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amefafanua kuwa limetokea kati ya saa 6 hadi 7 usiku wa kuamkia leo (Aprili 13,2025. "Ni kweli tukio lipo na amefariki dunia," amesema Mtambi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema ni baada ya gari la Mkurugenzi lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Bunda kugongana na lori. Amesema chanzo cha tukio hilo ni dereva wa gari lililokuwa limembeba Mkurugenzi aina ya Toyota Land Cruiser kumkwepa mwendesha baiskeli kisha kupoteza mwelekeo na kugongana na lori. "Tukio limetokea Bunda saa 7.30 usiku baada ya dereva wa gari aina ya Toyota Land Cruiser iliyombeba mkurugenzi kumkwepa mwendesha baiskeli na kugongana na lori kisha kupelekea vifo vya dereva na bosi wake,...

Dkt. Gwajima Ahimiza Serikali wa Mitaa Kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Mtoto

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Dkt. Dorothy Gwajima amesema serikali za mitaa ni kitovu cha utekelezaji wa mikakati ya ulinzi na usalama wa mtoto iwapo jamii itatoa taarifa kwa wakati kuhusu changamoto za kifamilia ambazo ni tishio kwa ustawi wa watoto Ili wataalamu wa ustawi wa jamii kwenye ofisi hizo waweze kushirikiana na familia au jamii husika kupata ufumbuzi wa pamoja kulingana na fursa zilipo serikalini na kwa wadau wanaoshirikiana na Serikali.  Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Mtaani mkoani Mtwara, Dkt. Gwajima amesema, "watoto hukimbilia kuishi na kufanya kazi mitaani kutokana kukosa ufumbuzi dhidi ya changamoto zinazowakabili huku kukiwa hakuna aliyetoa taarifa serikali za mitaa kabla ya mtoto kutoroka nyumbani Ili wataalamu wa ustawi wa jamii waweze kusaidia ufumbuzi". Aidha, amesema, kati ya Julai 2024 hadi Machi 2025 jumla ya  vipindi 140 vya elimu kwa umma vimetolewa kupitia redio za jamii huku, migogoro ya ndoa 16,095 ilifanyiwa ka...

Taded ya Waasa Wananchi Kupiga Kura

Na Richard Mrusha Mwenyekiti was Taasisi ya Demokrasia na Maendeleo Tanzania Democracy and Devoloment,TADED) Chalilla Kibuda ibuda leo April 12,2025 amesema swala la uchaguzi mkuu ni jukumu la kila mtanzania mwenye sifa za kipoga kura.  Amesema  wao kama Taasisi wamejipambanua kuhamasisha  watu kujitokeza kwenye uchaguzi maana kwakifanya hivyo watapata maendeleo  ambapo kuanzia ngazi ya kata Hadi Taifa. Ameongeza kuwa Kwa  kuhamasisha watu kushiriki katika uchaguzi  utaofanyika Oktoba mwaka huu ni haki ya kila mtu na asitokee mtu yeyote wa kada yeyote na kuwavunja mioyo watu . Kibuda amesema Katika uchaguzi  huu ni haki ya kila mwananchi kushiriki katika kuchagua viongozi wataodumu kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa Katiba  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amesema Uchaguzi huu kwa katiba hii hakuna chombo chochote kinachoweza kuzuia kutofanyika uchaguzi ambapo hata chama kilichopo madarakani hakiwezi kufanya hivyo. Ameongeza kuwa Hata h...