Skip to main content

Posts

Showing posts from November 16, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mhe.Mchengerwa:Rufaa 5,589 za Wagombea Zimekubaliwa

 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kati ya rufaa 16,309 za wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa zilipokelewa, rufaa 5,589 zimekubaliwa. Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Novemba 16, 2024, Waziri Mchengerwa amesema rufaa hizo ni pamoja na zilizowasilishwa baada ya muda wa nyongeza wa siku mbili na uamuzi wake umezingatia dosari ambazo zilisababisha kutoteuliwa kwao awali hazikuwa kubwa zinazoathiri matokeo yaliyokusudiwa na kanuni.  Aidha, amesema katika nafasi zinazogombewa vyama 18 vya siasa vimeweka wagombea katika nafasi 30,977 kati ya nafasi 80,430 sawa na asilimia 38.51 huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiweka wagombea katika nafasi zote.  Amesema katika nafasi za mwenyekiti wa kijiji zinazogombewa ni 12,280 ambapo vyama hivyo vimeweka wagombea katika nafasi 6,060 sawa na asilimia 49.35. Pia, amesema nafasi za mwenyekiti wa mtaa zinazogombewa ni...

Juliana Masaburi aomba Mifuko ya Mikopo iwafikie Vijana Wote

MBUNGE wa viti maalum kupitia vijana mkoa wa Mara Mhe. Juliana Didas Masaburi amesema Ofisi ya Waziri Mkuu ina Mifuko zaidi ya 71 yenye fursa za kuwawezesha vijana lakini haiwafikii walengwa katika kuondoa tatizo kwa ajira kwa kundi hilo kubwa nchini. Mh Masabari ametoa rai hiyo kwenye kongamano aliloliitisha kwa ajili kuangalia fursa  za kiuchumi kwa vijana wa mkoa wa Mara na kufanyika ukumbi wa CMG mjini Tarime Amewaambia Vijana zaidi ya 1,000 kutoka Wilaya zote Saba za Mkoa wa Mara na Mikoa ya jirani kuwa endapo mifuko hiyo kutoka ofisi ya waziri mkuu ingetumika kikamilifu ingweza kusaidia mitaji kwa vijana na hivyo kupunguza tatizo la ajira nchini. Katika kongamano hilo vijana walipata mafunzo kutoka kwa Wakufunzi na Wataalam wa Wizara ya Madini, Wizara ya Nishati, Wizara ya TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi kadhaa "Tutakuwa viongozi waongo tukiwaambia kuwa Serikali ya CCM au Serikali ya Awamu ya Sita itawaletea fedha mifukoni mwenu vijana kila siku au kila mwisho wa m...

Dkt.Biteko awataka Wahitimu Wasiogope Changamoto za Maisha baada ya Chuo

 *📌 Awahimiza kufanya uamuzi sahihi, kujibu maswali na dukuduku walizonazo* *📌 Apongeza ushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi katika maendeleo nchini* *📌 SAUT yamshukuru Rais Dkt. Samia kwa miongozo katika sekta ya elimu* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza wahitimu katika ngazi mbalimbali kutumia taaluma yao kufanya maamuzi sahihi yatakayowawezesha kupata majibu ya maswali na dukuduku walizonazo kuelekea maisha mapya. Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Novemba 16, 2024 katika Mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu Kishiriki, Stella Maris cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Mtwara.  Pamoja na kuwapongeza wahitimu kwa kuhitimu amewataka kutumia taaluma waliyoipata kuwa nyenzo katika utatuzi wa changamoto watakazokabiliana nazo maishani baada ya kuondokana na maisha ya chuo.  “ Wengine wanaendelea kujiuliza, nini kitafuata baada ya kuhitimu? Uelekeo utakuwa ni upi? na wengine wanasema hali s...

Rc Mtambi Awataka Maofisa Kilimo Kutoa Elimu ya Kilimo Mseto Kwa Wakulima

Fresha Kinasa- Mara. MKUU  wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi, amewaagiza Maofisa Kilimo  wote Mkoani humo kuhakikisha   wanapeleka elimu ya Kilimo mseto na uhifadhi wa mazingira  katika maeneo wanayofanyia kazi ili wananchi wazalishe mavuno yao kwa tija. Kanali Mtambi ameyasema hayo Novemba 16, 2024 wakati akifunga maonesho ya tisa ya Kilimo mseto yaliyofanyika kuanzia Novemba 14, 2024, hadi Novemba 16, 2024, katika kituo cha mafunzo  ya Kilimo mseto kilichopo kata ya Bweri Manispaa ya Musoma. Amesema,  kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, wakulima wanalojukumu la kuhakikisha wanalima Kilimo mseto kwa kutumia eneo dogo lakini wazalishe mavuno mengi na kutunza mazingira.  Hivyo ili Jambo hilo lifanikiwe Maofisa Kilimo wanapaswa wawajibike kutoa elimu kwa wakulima. "Maofisa Kilimo   pelekeni elimu kwa wananchi walime Kilimo mseto na pia watunze mazingira yao ikiwemo uoto wa asili kwa kupanda miti kwa wingi. Ili tukabiliane na mabadiliko...

Tarura Manyara Kufungua Barabara Mpya Km.109

#Wananchi wahamasishwa kutunza miundombinu ya barabara  Babati, Manyara Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Manyara ina mpango wa kufungua barabara mpya zenye urefu Km. 109 katika Wilaya ya Mbulu, Simanjiro pamoja na Babati  katika mwaka wa fedha  2024/2025. Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa TARURA Mkoa wa Manyara Mhandisi Salim Bwaya wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani hapo hivi karibuni. Mhandisi Bwaya amesema kwamba kilomita hizo za barabara zinaenda kuwanufaisha wananchi na kuwaletea manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa kuwarahisishia kupata huduma za kijamii kwa urahisi. “Mwaka huu wa fedha tuna mpango wa kufungua barabara katika wilaya  ya Mbulu (Km. 46), Simanjiro (Km. 41), pamoja na Babati (Km. 22) ambapo itajumuisha ujenzi wa barabara za lami(Km. 11.7),changarawe (Km. 251.4) pamoja na matengenezo ya barabara za udongo (Km. 385) na ujenzi wa vivuko vipatavyo 104," amesema. Amesema kwamba licha ya kufungua kilomita hizo za bar...