WAZIRI wa Madini Nchini Tanzania Anthon Mavunde Leo June 5,2026 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Serikali ya Urusi kwenye sekta ya madini ukiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili(Madini) na Mazingira wa Shirikisho la Urusi, *Mh. Tetenkin Dmitry Dmitrievich*. “Pamoja na kuendelea kukua kwa kasi kwa sekta yetu ya madini, Nchi yetu imefanikiwa kufanya utafiti wa kina kwa asilimia 16 pekee. Hivyo, iwapo tutaongeza eneo kubwa litakalokuwa limefanyiwa utafiti, kutatanua wigo wa taarifa zaidi za mashapo ya madini na kuvutia zaidi wawekezaji, Eneo hili la utafiti tunaona ni fursa kubwa ya kuanza nayo katika kuimarisha mashirikiano yetu na Serikali ya Urusi kutokana na hatua kubwa mliyopiga hususan katika utafiti wa kijiolojia na teknolojia ya kisasa kupitia maabara zenye vifaa bora” Tumezungumza juu uwepo wa Hati ya Makubaliano(MoU) baina ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) na Chuo Kikuu cha Urusi ambayo bado haijakamilika na kumwomba kuiwekea nguvu i...
Marato tv - Sauti ya Jamii