Skip to main content

Posts

Showing posts from October 28, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais wa caf aomboleza vifo vya wachezaji wa timu ya chavuma

 Wachezaji saba wa klabu ya Chavuma Town Council ya nchini Zambia wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa kwenye ajali ya basi wakati kikosi hicho kikielekea kwenye mechi ya ligi ya daraja la tatu, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo. Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Patrice Motsepe ametuma salamu za rambirambi kwa familia na Shirikisho la Soka Zambia kwa vifo hivyo.

Nirc yatimiza ahadi ya waziri Bashe ya kuwapatia mtambo wa umwagiliaji vijana wanaolima vitunguu songea

Na NIRC ;Ruvuma Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekabidhi mtambo wa umwagiliaji wenye thamani ya shilingi millioni 4.2 kwa Jacob Davis na wenzake wawili  wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji kwenye kijiji cha Nakahengwa halmashauri ya wilaya Songea Mkoani Ruvuma.  Wakulima waliokabidhiwa Mtambo wamejikita kuzalisha vitunguu ambapo Tume hiyo imetoa Mtambo huo ikiwa ni Utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe.  Waziri Bashe alitoa ahadi ya kuwasaidia vijana hao septemba 17 mwaka huu alipotembelea shamba lao akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa pamoja viongozi wengine. Akiwa kwenye shamba hilo,Waziri Bashe alivutiwa na kilimo cha vitunguu ambapo vijana hao walieleza changamoto zinazowakabili katika kilimo hicho ikiwemo ukosefu wa miundombinu ya uhakika ya umwagiliaji,hali inayochangia  kushindwa kutanua wigo wa kulima mashamba makubwa kutokana na hali duni ya kiuchumi.  Baada ya Waziri Bashe ku...

Majaliwa ateta na waziri wa uchumi wa urusi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Shirikisho la Urusi, Bw. Maxim Reshetnikov na kujadiliana naye masuala mbalimbali yakiwemo yanayogusa biashara, kilimo, usafirishaji, elimu, nishati na utalii. Akizungumza na Waziri Reshetnikov leo (Jumatatu, Oktoba 28, 2024) ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amemhakikishia Waziri huyo kwamba Tanzania ni mahali pazuri pa kufanya biashara kwa kuwa ni nchi tulivu na Mwenyezi Mungu ameiweka mahali pa kimkakati pa kuweza kufanya biashara. “Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipambanua kufanya maboresho kwenye biashara kati ya Tanzania na nchi marafiki, Urusi ikiwemo. Kupitia ziara hii, nina uhakika mtapata maelezo mazuri ambayo yatawatia moyo wa kuiamini Tanzania kwamba ni mahali pazuri pa kufanyia biashara,” amesema, Akielezea kuhusu fursa zilizopo nchini, Waziri Mkuu amesema Tanzania inapakana na bahari yenye bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga. “Ina maziwa ya Victori...

Rais Samia azidi kupata watetezi

Kiongozi wa Huduma ya Matengenezo ya Kiroho Ulimwenguni,Augustine Bilomo Maarufu kwa Jina la Mfalme Tengwa amekemea usaliti unaofanywa na baadhi ya viongozi dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza,Mfalme Tengwa amesema kuwa Rais Samia anajengewa fitina na watu wenye nia mbaya kwa lengo la kuzorotesha utawala wake. Amedai kuwa baadhi ya makundi ambayo yamekuwa yakimhujumu na kumchafua Rais Samia ni pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma,wafanyabiashara,Viongozi wa madhehebu ya dini na watu wa kada mbalimbali. ‘’Tanzania ina wasaliti,wanamfanyia hila Rais Samia ili aonekane ndiye anayetuma watu kuteka na kuuwa watu wakati si kweli,Mi mungu amenambia huyu mama ni ishara madhubuti ya Taifa hili ila kuna vitengo mbalimbali vinavyofanya kazi kinyume na Rais kwa nia ya kutaka kuuharibu uongozi wake’’alisema Mfamle Tengwa na kuongeza kuwa ‘’Rais Samia ni kiongozi wa kwanza nchini kuruhusu kufanyika kwa maandamano ya amani,Ma...

Tarura katavi yaboresha miundombinu ya barabara

 Katavi Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeendelea kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa kujenga barabara, vivuko na madaraja katika maeneo mbalimbali mkoani Katavi ili kuinua shughuli za kijamii na kiuchumi. Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Meneja wa TARURA Mkoa wa Katavi, Mhandisi Japhet Bengesi alisema, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa katika kuimarisha miundombinu ya barabara mkoani Katavi. Mhandisi Japhet amemshukuru Rais Samia kwa kuongeza bajeti ya TARURA mkoa wa Katavi kutoka Shilingi Bilioni 4 hadi kufikia Shilingi Bilioni 15 ambayo kwa kiasi kikubwa imesaidia kuimarisha mtandao wa barabara mkoani humo. "Tumeweza kufungua barabara mpya ambazo hazikuwepo kabisa zenye urefu wa Km 439, barabara za changarawe zimeongezeka kutoka Km 471 hadi Km 692 ambalo ni ongezeko la Km 221 na barabara za lami kutoka Km 36 mpaka Km 53 ambalo ni ongezeko la Km 17 ...