Skip to main content

Posts

Showing posts from October 25, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri mkuu aikabidhi Takukuru magari 88

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2024 amekabidhi magari mapya 10 ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 88 yaliyonunuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) ambayo yatasambazwa mikoani kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hiyo. Akitoa taarifa ya magari hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila amemweleza Waziri Mkuu kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani, TAKUKURU imepatiwa jumla ya Shilingi bilioni 30 za kununulia magari 195 ambapo 88 yameshanunuliwa. “Mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea na tunatarajia kuyapata hivi karibuni, tunaahidi kutatunza magari haya ili kuongeza tija katika utendaji wetu” Amesema  Bw. Crispin Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo wakati anafunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), hafla hiyo inafanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Waziri mkuu agawa fimbo nyeupe kwa watu wenye ulemavu wa kuona

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akigawa fimbo nyeupe kwa watu wenye ulemavu wa kuona alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe na Miaka 60 ya Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) ambayo kitaifa yamefanyika Mkoani Kilimanjaro jana Oktoba 25, 2024.

Waziri mkuu kufunga mafunzo ya awali Pccb

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo oktoba 26, 2024 anafunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, hafla hiyo inafanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa nishati Zanzibar aipa kongole Rea

*📌AISISITIZA KUENDELEA NA UHAMASISHAJI* *📌REA YAELEZEA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA NA USAMBAZAJI WA UMEME VIJIJINI* Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mhe. Shaib Kaduara ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuendelea kuhakikisha huduma za Nishati zinafika katika maeneo yote ya Vijiji Tanzania Bara. Ametoa pongezi hizo Jijini Dar es Salaam Oktoba 25, 2024 alipotembelea Banda la Wakala kabla ya kufunga Kongamano la 10 la Jotoardhi (ARGeo-C10). Mhe. Kaduara aliisisitiza REA kuhakikisha inaongeza nguvu katika suala la uhamasishaji ili kuwezesha wananchi umuhimu wa kubadilika na kuachana na matumizi ya nishati ambazo sio safi na salama kwa afya zao na kwa mazingira. "Hongereni mnafanya kazi nzuri, muhimu ni kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi waelewe umuhimu wa kubadilika na kuachana na matumizi ya Nishati chafu," alielekeza. Awali akitoa maelezo ya majukumu ya REA, Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Waka...

Majaliwa:serikali yatenga shilingi billioni 20 kukopesha wenye ulemavu

*Asisitiza hakuna sababu ya kumficha mtoto mwenye ulemavu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga shilingi bilioni 20.21 kwa ajili ya watu wenye ulemavu ikiwa ni mikopo yenye masharti nafuu na isiyokuwa na riba inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri  Amesema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 25, 2024) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe na Miaka 60 ya Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Mkoani Kilimanjaro.  “Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Halmashauri zilitenga shilingi bilioni 16.14, hili ni ongezeko kubwa. Viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu wekeni utaratibu ili wanachama wenu waweze kunufaika na fursa hii ambayo Serikali imeitoa kwa watu wenye ulemavu.” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Miradi (UNOPS)imewezesha kupatikana ruzuku ya shilingi bilioni 8.2 kwa ajili...

Mtanzania kuwa Mkurugenzi Benki ya Dunia

Benki ya Dunia, imemchagua Mtanzania, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika inayojumuisha nchi 22 ikiwemo Tanzania, nafasi ambayo Tanzania imewahi kuihudumu miaka 54 iliyopita. Uamuzi wa Dkt. Kibwe kuikwaa nafasi hiyo nyeti katika Taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani, umetangazwa katika Mkutano wa Mwaka wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Benki ya Dunia, uliofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani ambapo Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha Duniani IMF na Benki ya Dunia inafanyika. Kabla ya kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki hiyo atakayesimamia Kanda Namba Moja ya Afrika, Dkt. Kibwe alihudumu katika Ofisi hiyo ya Bodi kama Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Mshauri na Mshauri Mwandamizi kwa zaidi ya miaka saba, tangu mwaka 2017. Akizungumza Jijini Washington D.C, baada ya kutangazwa kuchukua nafasi hiyo, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe amesema kuwa ataitumia nafasi hiyo kusimamia uendeshaji wa Ben...

Waziri mkuu amwakilisha Rais Samia Maadhimisho ya siku ya fimbo nyeupe

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 25, 2024 amewasili mkoani Kilimanjaro ambapo anamwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe na Miaka 60 ya Chama cha Wasioona Tanzania (TLB). Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe huadhimishwa kila Oktoba 15 kwa lengo la Kuelimisha jamii kuhusu haki na uwezo wa watu wenye ulemavu wa kuona, Kutambua umuhimu wa fimbo nyeupe katika kusaidia watu wenye ulemavu wa kuona kusafiri kwa usalama na uhuru na hatimaye kufikia malengo yao. Aidha, Siku hiyo pia ina lengo la kuhamasisha ujumuishaji wa watu wenye ulemavu wa kuona katika jamii na kuhakikisha wanapata fursa sawa katika elimu, ajira, na huduma zote nyingine. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Upatikanaji wa Teknolojia Saidizi na Fikivu ni Mkombozi kwa Uchumi Endelevu kwa Mtanzania asiyeona.”