WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo iweke utaratibu wa kuziwezesha taasisi zinazojihusisha na kilimo kwa kuzipatia zana za kisasa za kilimo ili kukuza sekta hiyo. Amesema kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza tija katika shughuli za kilimo zinazofanywa na taaaisi hizo. “Mitambo hii ya kupandia, kuvunia pamoja na umwagiliaji ina gharama kubwa sana, lakini Wizara yetu ya Kilimo ikiweka utaratibu mzuri wa kuziwezesha hata kwa mkopo itazisaidia kuzalisha kwa tija.” Ametoa agizo leo (Jumapili, Agosti 03, 2025) wakati akizungumza na wadau wa ushirika na wananchi waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Kitaifa yaliyofanyika katika Kijiji cha Ushirika, kwenye viwanja vya maonesho ya NaneNane, Nzughuni, jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wakulima kwa mwaka 2025. Amesema taasisi kama Magereza, JKT ambazo zinafanya shughuli za kilimo zikipatiwa zana hizo kwa mikopo, zitawawezeshwa kuwa na teknolojia za kisasa jambo ambalo wasingeweza kul...
Marato tv - Sauti ya Jamii