Skip to main content

Posts

Showing posts from December 16, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Akagua Uharibifu wa Miundombinu

 WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 17, 2025 akizungumza na wakazi wa eneo la Tunduma mkoani Songwe ambapo yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua uharibifu wa miundombinu ya umma na mali binafsi zilizoharibiwa na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025. Akizungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewaagiza Watendaji Wakuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na TARURA kufanya tathimini ya miradi yote ambayo malipo ya awali yameshafanyika na hatua za ujenzi zilizofikiwa katika miradi hiyo.  Pia amewaagiza kuangalia kama utekelezaji wa miradi hiyo unaendana na kiwango cha fredha ambacho kimeshatolewa.

TRA Yakamata Mafuta ya Magendo Bandari ya Kunduchi

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mnamo Desemba 16, 2025, imekamata shehena kubwa ya mafuta ya kupikia ya magendo, jumla ya madumu 23,755, yaliyokuwa yakiingizwa nchini kinyume na taratibu kupitia Bandari ya Kunduchi, jijini Dar es Salaam. Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, alizungumza mara baada ya zoezi hilo na kueleza kuwa bidhaa hizo za magendo zimekuwa tishio kwa uchumi wa nchi, kwa kuwa zinapunguza mapato ya serikali na kudhoofisha ukuaji wa viwanda vya ndani. Aidha, aliongeza kuwa bidhaa hizo zisizopitia ukaguzi wa mamlaka husika huweza kuwa hatari kwa afya za walaji, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushiriki katika kuzuia biashara hiyo haramu. TRA imesisitiza kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika wa biashara za magendo, huku ikihamasisha wananchi kushirikiana katika kutoa taarifa ili kulinda uchumi wa Taifa.

Dkt. Mwigulu Akagua Uharibifu Mizani ya Magari Mpemba, Songwe.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 17,2025 amekagua uharibifu uliofanyika katika mizani ya magari iliyopo Mpemba, mkoani Songwe, uharibifu huo ulitokana  na vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu yupo mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi

Waziri Mkuu Kufanya Ziara za Kikazi Songwe na Mbeya

WAZIRI MKUU,  Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 16, 2025 amewasili katika uwanja wa ndege wa Songwe. Mheshimiwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu  atakuwa na ziara ya kikazi katika mikoa ya Songwe na Mbeya tarehe 17 hadi 19, 2025.

Mongella Akiwa na Viongozi Mbalimbali wa Kitaifa Wakipunga Mikono Kuashiria Kuagana na Jenista Mhagama

  Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo tarehe 16 Desemba, 2025, amejumuika na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, pamoja na wananchi, katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama, yaliyofanyika Kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma. Akiwasilisha salamu za Katibu Mkuu wa CCM, katika shughuli hiyo iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Ndugu Mongella alisema kuwa Mhe. Jenista alikuwa kada na mwanachama mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi katika kipindi chote cha uhai wake, akiaminiwa kuwatumikia wanachama na wananchi, kupitia dhamana mbalimbali za uongozi ndani ya Chama na Serikali, kwa uadilifu na unyenyekevu mkubwa.

Dkt. Mwigulu Ashiriki Mazishi ya Mhe. Jenista Mhagama

  _Atoa maagizo kwa Mkandarasi wa barabara ya Kitai-Ruanda._ Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba leo Desemba 16, 2025 ameshiriki katika Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika katika Kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Akizungumza katika mazishi hayo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed kumsimamia mkandarasi anayejenga barabara ya Kitai hadi Ruanda ili akamilishe ujenzi wa barabara hiyo muhimu kwa wakazi wa mkoa huo. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema tayari Serikali ilikwisha kutoa fedha za ujenzi wa barabara hiyo kwa kutambua umuhimu wake kwenye uchumi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla. “Ni dhahiri kabisa kwamba kasi ya ujenzi hairidhishi nikutake mkuu wa mkoa, mwite mkandarasi huyu mara baada ya shughuli hii, mwambie alishapokea fedha sasa afanye kazi ionekane, kama ameshatumia pesa hiyo kwenye kazi nyingine kamata passport yake asitoke mpaka kazi hii ikamilike” Makamu w...

Balozi Matinyi akutana na Mfalme wa Sweden

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mheshimiwa Mobhare Matinyi, akisalimiana na Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden, kwenye Kasri la Mfalme jijini Stockholm, tarehe 9 Desemba, 2025. Kushoto ni Binti Mrithi wa Ufalme, Victoria, katikati ni Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Balozi Maria Christina Lundqvist, na kulia ni Mke wa Balozi, Yvonne Matinyi. Katika mazungumzo yao mafupi, Mfalme Gustaf na Balozi Matinyi walijadiliana kuhusu uimarishaji wa uhusiano baina ya nchi hizo mbili, hususani, katika nyanja za biashara, uwekezaji na utalii. (Picha kwa hisani ya Kasri la Mfalme).