Na Angela Sebastian-Bukoba Serikali imetenga shilingi bilioni 8 kupitia wakala wa Nishati viiiiiji (REA) kwa ajili ya kusambaza umeme ndani ya visiwa 118 vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchi nzima,ili kuwafikishia huduma za nishati ya umeme wananchi wote wanaoishi maeneo ya visiwa na yale ambayo siyo rahisi kufikiwa na gridi ya Taifa. Mkurugenzi wa teknolojia ya Nishati jadidifu mbadala kutoka REA mhandisi Advera Mwijage ameeleza hayo wakati wa ziara ya bodi ya wakurugenzi wa wakara hiyo walipotembelea moja ya kisiwa ambacho kiko kati ya visiwa 118 vinavyotakiwa kupitiwa mradi huo na kuongea na wananchi kisha kukagua maendeleo ya mradi. Bodi ikiongozwa na Mwenyekiti wake balozi meja jenerali mstaafu Jacob Kingu jana ilitembekea katika kisiwa Cha Musira kilichopo ndani ya ziwa Viktoria Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambapo ni moja ya kisiwa kilichotengewa zaidi ya shl.bil. 2 na serikali ili kupeleka nishati katika eneo hilo...
Marato tv - Sauti ya Jamii