Mtanda ahimiza matumizi sahihi ya magari ya serikali

GEORGE MARATO TV
0


 Serikali imeipatia wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)Mkoa wa mwanza vitendea kazi ikiwemo magari manne pamoja na pikipiki nne ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa wakala huo.

Vitendea kazi hivyo vimegharimu zaidi ya shilingi millioni mia nane na vimekabidhiwa kwa Ruwasa na Mkuu wa mkoa wa mwanza Said Mtanda ambaye amehimiza utunzaji wake pamoja na kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara.


Mtanda amesema kuwa hatua hiyo itawezesha magari na pikipiki zilizotolewa kutoa huduma endelevu.

‘’Serikali ya Rais Samia inaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za maji nchini pamoja na kuongeza vitendea kazi na leo tumeona magari manne ya kisasa,kwa mfano haya yanakwenda sengerema na ukerewe,hizi pickup sijawahi kuziona kabisa na naamini kabisa meneja huko ukerewe atafurahi sana’’alisema Mtanda na kuongeza kuwa

‘’Magari ya serikali lazima yafanye kazi inayokusudiwa na pale tunapoona kwamba magari yale yamefika ukomo tufuate utaratibu wa wa kuyauza kwa watumishi wanaoweza kuyanunua ili kuboresha maisha yao sio dhambi lakini tusiyaharibu kwa makusudi ili tujikopeshe’’

Aidha Mtanda amesema wakuu wa Taasisi za umma wanaowajibu wa kudhibiti mienendo ya madereva pamoja na usimamizi wa magari ili kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya serikali.



Pia amewaasa watumishi wa Ruwasa mwanza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya serikali ya kutoa huduma bora ikiwemo kufikisha huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 85 ya wananchi waishio vijiji ifikapo Juni mwaka 2025.




Naye meneja wa Ruwasa Mkoa wa mwanza Mhandisi Godfrey Sanga ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuIpatia wakala huo pikipiki nne na magari manne pamoja na kuahidi kutoa magari mawili kwa ajili ya wilaya mbili zilizosalia ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

‘’Magari matatu yanakwenda kwenye wilaya za Kwimba,Misungwi na Sengerema na ofisi ya mkoa pia imepata gari moja huku pikipiki nne zikienda kwenye wilaya sengerema,pikipiki na magari haya yatatusaidia sana kwenye kusimamia utoaji wa huduma ya maji vijijini’’Alisema Mhandisi Sanga na kuongeza kuwa

‘’Hivi vyombo vya usafiri vitatuwezesha kuwafikia wananchi ikiwemo kwenda kwenye maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya maji ili tufanye usanifu kwa ajili ya kutengeneza miradi mipya kwenye vijiji vilivyobaki na ninaahidi kuhakikisha vyombo hivyo vya usafiri vinatunzwa’’  

Mkoa wa Mwanza kwa sasa inatoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi millioni 2.4 waishio vijijini sawa na asilimia 72 ambapo idadi hiyo inatarajia kufikia asilimia 86 ifikapo juni mwaka 2025 pindi miradi 55 inayotekelezwa na serikali kwa gharama ya shilingi billioni 146 itakapokamilika.

‘’Miradi hiyo inatarajia kuhudumia watu takriban laki saba ambao ni sawa na asilimia 14 ya waishio vijijini mkoani mwanza na hivyo kutoka kwenye asilimia 72 tutaenda asilimia 86 ifikapo juni 2025,kama mnavyofahamu ilani ya CCM ya mwaka 2020 hadi 2025 inatutaka tufikishe huduma ya maji kwa asilimia 85’’alisema Mhandisi Sanga

Kabla ya kutolewa kwa magari hayo,Ruwasa Mwanza ilikuwa inatumia magari yaliyonunuliwa miaka 15 iliyopita na hivyo kulazimka kuingia gharama kubwa ya matengenezo ya mara kwa mara kutokana na magari hayo kuwa chakavu. 












Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top