Jamii Yashauriwa Kutunza Mazingira Ili Kukabiliana na Mabadiriko ya Tabia Nchi

GEORGE MARATO TV
0

 


Na Fesha Kinasa, Mara. 

JAMII imeshauriwa kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira na uoto wa asili kwa kutenga maeneo ya  kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa na athari kwa viumbe hai.  

Hayo yamesemwa Novemba 6, 2024, na Mdau wa Mazingira Robinson Wangaso wakati akikabidhi Miche ya miti 150 katika shule ya Secondary Salama  iliyopo Wilaya ya Bunda  Mkoani  mara.

Wangaso amesema kuwa, ili kuhakikisha mazingira na  uoto wa asili unalindwa kwa manufaa endelevu ya Mwanadamu na viumbe hai.   Ni  jukumu la Wananchi  wote  kupanda miti na kuitunza vyema katika maeneo yao na kushiriki katika agenda ya serikali ya  kuifanya Tanzania iwe ya kijani. 


Ameihimiza pia  Jamii kuzingatia matakwa ya serikali na Wadau wa Mazingira kwa kuachana na tabia zinazoathiri mazingira ikiwemo kukata miti ovyo, kuchoma mkaa na kulima maeneo ya vyanzo vya maji yaliyohifadhiwa kwani athari zake ni pamoja na kusababisha ukame. 

Pia, ametoa wito kwa Wanafunzi katika shule za Msingi, Sekondari na vyuo mbalimbali waendelee kujenga utamaduni   wa kupenda  kupanda miti na kuitunza katika taasisi hizo. Kwani kutawafanya wawe mabalozi Waziri wa mazingira katika maisha yao.  

Katika hatua nyingine, Wangaso amewaomba wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo watakaohitimu masomo yao na kupata ufaulu wa Kati wa kusoma vyuo wasikae mitaani bali watafute fursa ya kujiunga na vyuo mbalimbali vya Kati kupata ujuzi kwa manufaa yao. Huku watakaofaulu akiwahimiza kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano. 

"Mtakaoshindwa kuendelea na kidato cha tano,  msikae tu kijijini hapa bila kazi ya kufanya vipo vyuo mbalimbali tafuteni mjiunge msome  fani mbalimbali. Mkipata ujuzi vyuoni utasaidia kujiajiri wenyewe  na mtakaobahatika mtaweza kuajiriwa pia."amesema Wangaso. 

Kwa upande Wake Makamu Mkuu wa Shule hiyo Cosmas Chegela amemshukuru Wangaso kwa kuunga mkono juhudi za serikali za  utunzaji wa mazingira shuleni hapo, huku akiahidi usimamizi madhubuti wa miti hiyo.

"Tunakushukuru kwa kutuletea Miche hii ya miti, nikuhakikishie tutaitunza na kuisimamia kikamilifu na pia elimu ya utunzaji mazingira uliyoitoa kwa wananfunzi wetu naamini watakwenda kuifanya kazi kwa kutoa hamasa kwa Wazazi  na walezi ili walau kila familia ipande miti na hata serikali imekuwa ikisisitiza Jambo hili muhimu."amesema Cosmas.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top