Skip to main content

Posts

Showing posts from November 17, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT. MWIGULU MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA COSTECH

  Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Novemba 18, 2026, ni mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 40 ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Hafla hiyo inafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

RC BATILDA AMKABIDHI WAZIRI SULEIMAN AMEIR ZAWADI YA "SAA YA MKONGE"

  Na MASHAKA MHANDO, Tanga MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian, amefanya tukio lenye ujumbe mzito wa kiuchumi na kitamaduni baada ya kumkabidhi zawadi maalumu ya saa ya ukutani Waziri wa Vijana kutoka Zanzibar, Mhe. Suleiman Ameir, katika ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa vijana unaoendelea jijini Tanga. Mkutano huo wa kimataifa unajikita katika kujadili na kufungua fursa za vijana kupitia mpango maalumu wa kimataifa wa Global Opportunity Youth Network (GOYN), ukiwa unawakutanisha wadau mbalimbali ili kusaka mikakati ya kuwakwamua kiuchumi vijana. Zawadi hiyo iliyomkabidhi Waziri Ameir haikuwa ya kawaida; ni saa ya kipekee iliyotengenezwa kwa ustadi mkubwa wa mikono (handicraft) ikitumia malighafi ya mkonge, zao ambalo limekuwa uti wa mgongo wa Mkoa wa Tanga. Saa hiyo imetengenezwa na vijana wazawa kupitia kituo cha Tanga Sisal Incubation Centre, kituo kinachosimamiwa kwa karibu na Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB). Akieleza sifa na maana ya zawadi hiy...

GHATI CHOMETE AENDELEA NA ZIARA YA KIKAZI CHINA

  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Ghati Zephania Chomete, leo Novemba 17, 2026, ameendelea na ziara ya kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo katika Jiji la Chengdu, nchini China. Ziara hiyo ni sehemu ya shughuli za kamati katika kutekeleza majukumu yake ya kibunge yanayohusu sekta za viwanda, biashara, kilimo na mifugo, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika maeneo hayo. Ujumbe huo unaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Deodatus Mwanyika, ukiambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, pamoja na baadhi ya Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Serikali. Kupitia ziara hiyo, Mhe. Chomete anaendelea kushiriki katika shughuli za ujumbe huo, akiwa sehemu ya wajumbe wanaotekeleza majukumu ya kamati katika ziara hiyo nchini China.

MTAMBI AIPONGEZA MNUAT KUBADILI TASWIRA YA BUTIAMA KUPITIA MIUNDOMBINU YA KISASA

  MKUU wa Mkoa wa Mara, Brigedia Jenerali Evans Alfred Mtambi, ameipongeza Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MNUAT) kwa maendeleo makubwa ya ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho, akieleza kuwa uwekezaji huo umechangia kubadilisha taswira ya Wilaya ya Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla. Mtambi ametoa pongezi hizo leo, Novemba 17, 2026, alipompokea na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha MNUAT, Philemon Luhanjo, aliyefika mkoani Mara kwa ajili ya kushiriki kikao cha Baraza la Chuo. Akizungumza katika mapokezi hayo, Mtambi amesema chuo hicho kimepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake, hususan katika ujenzi wa miundombinu inayowezesha udahili wa wanafunzi katika Kampasi Kuu ya Butiama na Kampasi ya Tabora. “Kuna maendeleo makubwa sana ambayo yamefikiwa na chuo, ikiwemo majengo ya Kampasi Kuu ambayo yamesaidia sana kubadilisha muonekano wa Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla,” amesema Mtambi. Amesema hatua nyingine ...

TANZANIA YACHAGULIWA TENA KWENYE BARAZA LA ITU KWA MUHULA WA PILI MFULULIZO, 2027–2030

  Na Mwandishi Wetu  DOHA, Qatar Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechaguliwa kwa mara ya pili mfululizo kuwa Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) kuanzia 2027–2030, baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika tarehe 16 Novemba, 2026 katika Mkutano Mkuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU - PP 26). Ushindi huu unaashiria na kuthibitisha dhamira ya nchi katika kuendeleza mawasiliano ya simu duniani na maendeleo ya kidijitali. Nchi Wanachama 175 wa ITU walipiga kura katika mkutano huo, na kuchagua Baraza la Wajumbe 48 kwa miaka minne ijayo kuanzia 2027-2030. Viti kumi na vitatu kati ya hivyo vimetengwa kwa Kanda D, Afrika ambapo Tanzania ilipata nafasi ya kuwa mjumbe kwenye baraza hilo kwa kura 131. Serikali inaendelea kutumia fursa hii kuchangia kwa ufanisi katika uongozi wa kimataifa wa TEHAMA huku ikikuza matarajio ya kidijitali ya Tanzania, Afrika na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla. Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Mawasili...

KUDOS TO DR SAMIA'S GOVERNMENT AS TANZANIA SECURES FOUR MORE YEARS ON ITU COUNCIL

By Prosper Makene  President Samia Suluhu Hassan's Government has secured four more years on the Council of the International Telecommunication Union (ITU) after Tanzania was re-elected for a second consecutive term, 2027–2030, with 131 votes from 175 Member States at the ITU Plenipotentiary Conference (ITU PP-26). The election took place on 16 November 2026 in Doha, where Member States voted to choose 48 Council Members to serve for the next four years. Thirteen of those seats were allocated to Region D, Africa, and Tanzania secured one of them with a commanding vote. For President Samia's Government, the result is a clear vote of confidence in Tanzania's digital transformation agenda — an agenda focused on expanding broadband infrastructure, promoting innovation, improving public services through technology, and ensuring inclusive access for rural and underserved communities. The ITU Council serves as the Union's governing body between Plenipotentiary Conferences. It ...

WAZIRI WA ULINZI AKUTANA NA MEJA JENERALI MSTAAFU ZAWADI MADAWILI, JENERALI WA KWANZA MWANAMKE AFRIKA MASHARIKI

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 16 Novemba 2026, amemtembelea na kufanya mazungumzo na Meja Jenerali Mstaafu Zawadi Madawili katika makazi yake yaliyopo Upanga, jijini Dar es Salaam. Meja Jenerali Mstaafu Zawadi Madawili ana historia ya kipekee katika tasnia ya ulinzi na usalama, akiwa mwanamke wa kwanza katika Afrika Mashariki kufikia cheo cha Meja Jenerali, hatua inayodhihirisha mchango wake mkubwa katika utumishi wa kijeshi na ulinzi wa Taifa. Mazungumzo baina ya Waziri Dkt. Nyansaho na Meja Jenerali Mstaafu Madawili yalilenga kumjulia hali pamoja na kubadilishana uzoefu kuhusu safari yake ya utumishi wa kijeshi, mafanikio aliyoyapata na mchango wake katika kulinda na kuitumikia nchi. Aidha, ziara hiyo imetoa fursa ya kutambua na kuthamini mchango wa Meja Jenerali Mstaafu Madawili katika historia ya Jeshi na nafasi yake kama mfano wa kuigwa kwa wanawake katika utumishi wa kijeshi na uongozi.