Skip to main content

Posts

Showing posts from November 19, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAZIRI WA ULINZI AZINDUA MFUMO WA KIDIGITALI WA NGOME SACCOS

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), amezindua rasmi mfumo wa kisasa wa kidigitali wa Ngome SACCOS Limited, unaolenga kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wanachama. Uzinduzi huo  umefanyika 19 Novemba, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa Mkutano Mkuu wa 21 wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Brigade Mess. Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Nyansaho amepongeza uongozi wa Ngome SACCOS kwa kutumia teknolojia katika kuboresha huduma, akisisitiza kuwa Serikali inahimiza taasisi za fedha na vyama vya ushirika kuimarisha mifumo ya kidigitali ili kuongeza uwazi, kupunguza urasimu na kuwapatia wanachama huduma kwa haraka na ufanisi. Mfumo huo unatarajiwa kupunguza matumizi ya karatasi, kuondoa makosa ya kibinadamu na kuimarisha usalama wa kumbukumbu za wanachama. Mwenyekiti wa Bodi ya Ngome SACCOS amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kujenga taasisi imara ya kifedha, yenye uwezo wa kukidhi ongezeko la wa...

MBUNGE MGORE AONGOZA JITIHADA ZA TANZANIA KUTAFUTA SULUHISHO LA GHARAMA ZA UENDESHAJI WA RELI

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Mjini na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Mgore Miraji Kigera, ni miongoni mwa viongozi wanaoshiriki ziara ya kikazi nchini Italia yenye lengo la kujifunza teknolojia na mifumo ya uzalishaji wa vifaa vya reli, ili kutathmini uwezekano wa Tanzania kuanzisha kiwanda cha ndani kitakachopunguza gharama za uendeshaji na kuimarisha ufanisi wa huduma za usafiri wa reli. Ziara hiyo inalenga kupata uzoefu wa teknolojia ya kisasa katika uzalishaji wa reli, mifumo ya kubadilishia njia za treni (Switches), vipuri na vifaa vingine muhimu vinavyotumika katika ujenzi, matengenezo na uendeshaji wa miundombinu ya reli. Katika ziara hiyo, Mhe. Kigera ameungana na ujumbe wa Kamati kutembelea kiwanda cha RFI (Rete Ferroviaria Italiana), kilichopo Pontassieve nchini Italia, kinachojihusisha na utengenezaji wa vifaa na mifumo mbalimbali inayotumika katika sekta ya reli. Kupitia ziara hiyo, imelenga kujifunza mifumo ya uzalishaji na uendeshaji wa kiwanda hich...

MBUNGE WA JIMBO LA CHAMWINO AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI, ASISITIZA AMANI NA MSHIKAMANO

  CHAMWINO Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, Mhe. Dkt. Netho Ndilito, amewataka viongozi wa dini katika jimbo hilo kuendelea kutumia nafasi zao kuhamasisha umoja, amani, upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi ili kudumisha mahusiano mema katika jamii. Dkt. Ndilito ameyasema hayo Novemba 19, 2026, alipokutana na kufanya kikao na viongozi wa dini wa Jimbo la Chamwino, ambapo amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kuendelea kuwaelimisha waumini na jamii kwa ujumla kuhusu kudumisha amani na mshikamano. "Twendeni tukasisitize kwa watu wetu kuhakikisha umoja, amani, upendo na mshikamano katika jamii zetu vinaendelea kuimarika," amesema Dkt. Ndilito. Aidha, amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea kuwahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao, akieleza kuwa maendeleo yanahitaji ushirikiano kati ya Serikali na wananchi. "Serikali itafanya kwa kipande chake, lakini mwananchi naye ana namna ya kushiriki katika shughuli za maen...

NCHI ZA EAC ZATAKIWA KUPITIA MIKAKATI YA ULINZI ILI KUKABILIANA NA VITISHO VIPYA VYA KIUSALAMA

  Mabadiliko ya hali ya usalama katika eneo la Afrika Mashariki yanazitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuendelea kupitia na kuimarisha mikakati yao ya ulinzi ili kukabiliana ipasavyo na vitisho vipya na vinavyovuka mipaka ya nchi. Wito huo umetolewa Novemba 19, 2026, wakati wa Mkutano wa Kamati ya Ushauri kuhusu Ushirikiano katika Masuala ya Ulinzi uliofanyika Kampala, Uganda, ambapo washiriki wameeleza kuwa kulinda amani na usalama wa kikanda kunahitaji juhudi za pamoja, uratibu madhubuti na ushirikiano wa karibu kati ya nchi wanachama. Kamati hiyo, inayojumuisha Makatibu Wakuu wa Wizara za Ulinzi na Wakuu wa Majeshi kutoka nchi wanachama, imesisitiza kuwa changamoto za kiusalama zinazovuka mipaka, ulinzi wa njia za pamoja za biashara pamoja na majanga ya kibinadamu yanahitaji mikakati inayotekelezwa kwa ushirikiano ili kudumisha amani, utulivu na kulinda maendeleo ya eneo hilo. Tanzania inashiriki mkutano huo kupitia mwakilishi wake, Meja Generali Michael ...

CHATANDA AWASHUKURU WANAWAKE PEMBA KWA KUTEKELEZA MPANGO MKAKATI WA UWT

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amewapongeza na kuwashukuru wanawake wa Pemba kwa mchango wao katika kutekeleza Mpango Mkakati wa UWT, uliolenga kuhamasisha ushiriki wa wanachama na kuimarisha maandalizi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Akizungumza Novemba 19, 2026, katika mkutano wa ndani na wanawake pamoja na wanachama wa CCM Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, Chatanda amesema ushiriki na kujituma kwa wanawake hao katika kutekeleza mpango huo ulikuwa sehemu ya juhudi za pamoja zilizochangia matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2025, ambapo CCM ilipata ushindi. Amesema wanawake wameendelea kuwa sehemu muhimu katika shughuli za Chama, hivyo amewataka kudumisha mshikamano, umoja na ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya UWT na kuendeleza shughuli za CCM katika maeneo yao. Aidha, Chatanda amewahimiza wanachama wa CCM kuendelea kuhamasishana kuhusu usajili wa wanachama wapya pamoja na kulipia ada ...