Skip to main content

Posts

Showing posts from November 22, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MISS WORLD APAMBWA KWA KHANGA, AENDA SOKONI

  Mrembo wa Dunia (Miss World 2026), Joheirry Molla, amevalishwa khanga, vazi la asili linalotambulisha utamaduni wa Pwani, wakati akiendelea na ziara yake hapa nchini. Miss Molla akiwa pamoja na warembo wenzake ametembelea kikundi cha Mamas of Zanzibar, kinachojihusisha na upishi wa vyakula vya asili pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi. Katika ziara hiyo, Miss World na wenzake pia wametembelea Soko la Chuini, Zanzibar, ambako wamenunua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya vyakula vya asili, ikiwa ni sehemu ya kujifunza na kufurahia utamaduni wa Tanzania.

SHILINGI BILIONI 434 KUKAMILISHA UJENZI BANDARI YA KISIWA MGAO - PROFESA MBARAWA

  Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema uwekezaji wa shilingi bilioni 434 katika ujenzi wa Bandari ya Kisiwa Mgao, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, utakuwa suluhisho la changamoto ya kuchanganyika kwa shehena chafu na mizigo ya kawaida katika Bandari ya Mtwara, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia ubora na thamani ya fedha katika utekelezaji wa mradi huo. Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo Jumapili, Novemba 22, 2026, alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo, akieleza kuwa itakuwa mahususi kwa kuhudumia shehena chafu zikiwemo saruji, mbolea na makaa ya mawe, hivyo kuboresha ufanisi wa shughuli za upakuaji na upakiaji wa mizigo. Amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 300 na upana wa mita 40, huku akipongeza ubunifu wa Serikali wa kuanzisha tozo maalumu ya miundombinu (Infrastructure Fee), inayowezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi ya bandari na kurahisisha malipo kwa wakandarasi. “Kwa mara ya kwanza unamuuliza mk...

PRESIDENT SAMIA JETS OFF TO ETHIOPIA FOR CPHIA 2026

By Prosper Makene  Tanzania President Dr. Samia Suluhu Hassan, departed the country today, Sunday, 22 November 2026, from Kilimanjaro International Airport (KIA) for a two-day working visit to Addis Ababa, Ethiopia, where she will join African leaders for the Fifth International Conference on Public Health in Africa (CPHIA 2026). President Samia was seen off at KIA by various leaders before boarding flight to the Ethiopian capital.  Her departure marks a diplomatic engagement aimed at strengthening Tanzania's role in continental health diplomacy. While in Addis Ababa, the Head of State will participate in the high-level deliberations of CPHIA 2026, which brings together African heads of state, health ministers, scientists, researchers, health experts and development partners to discuss strategies for strengthening public health systems across the continent. The conference, now in its fifth edition, has become Africa's premier platform for sharing scientific evidence, innovatio...

MH DKT SAMIA SULUHU HASSAN AKIWASILI ADDIS ABABA

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 22 Novemba, 2026 kwa Ziara ya Kikazi ya siku mbili. akiwa Addis Ababa, Mhe. Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), pamoja na kuzindua Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika.

DKT. MWIGULU AAGIZA KUONGEZWA KASI YA UJENZI WA BARABARA YA BIGWA–KISAKI

  *_▪ Asema Serikali imeboresha utaratibu wa upatikanaji wa fedha za miradi ya barabara_* *_▪ Atarejea kukagua maendeleo ya ujenzi_* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amemtaka mkandarasi anayejenga sehemu ya barabara ya Bigwa–Mvuha–Kisaki, yenye urefu wa jumla wa kilomita 133, mkoani Morogoro, aongeze kasi ya ujenzi kwa kuhakikisha mitambo na wataalamu wanaohitajika wanafika eneo la mradi. Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo, (Jumapili, Novemba 22, 2026), wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Bwakila Chini, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, mkoani Morogoro. Amesema amepita katika barabara hiyo na kujionea hali yake, huku akieleza kuwa ziara yake imelenga kuongeza msukumo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. “Kuona kwenye makaratasi ni tofauti na kuona kwa macho. Kuona kwenye taarifa ni tofauti na kuona saiti kama leo ambavyo nimeiona mwenyewe barabara hii,” amesema. Waziri Mkuu amekiri kuwa ujenzi wa barabara hiyo umechelewa, lakini ameeleza kuwa u...

RAIS SAMIA KUELEKEA ETHIOPIA KUZINDUA MPANGO WA KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO AFRIKA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 22, 2026, anaondoka nchini kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, itakayomuweka katika nafasi muhimu ya kushiriki juhudi za kikanda za kuboresha afya ya mama na mtoto barani Afrika. Akiwa Kinara wa Umoja wa Afrika wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Rais Dkt. Samia anatarajiwa kushiriki Mkutano wa Tano wa Kimataifa wa Afya ya Umma Barani Afrika (CPHIA 2026), pamoja na kuzindua Mpango Elekezi wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto Barani Afrika, utakaofanyika Novemba 23, 202 Mpango huo unalenga kuimarisha juhudi za nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika kufikia malengo makuu matatu yanayofahamika kama Sifuri Tatu (Three Zeros), ambayo ni kuhakikisha kila mjamzito anajifungulia katika kituo cha kutolea huduma za afya chini ya uangalizi wa mtaalamu, kutokomeza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga vinavyoweza kuzuilika, pamoja na kuhakikisha kila mtoto anapata hudum...