Serikali Yatenga Bilioni 8 Kusambaza Umeme Ndani ya Visiwa 118 Nchi Nzima

GEORGE MARATO TV
0



 Na Angela Sebastian-Bukoba

Serikali imetenga  shilingi bilioni 8 kupitia wakala wa Nishati viiiiiji (REA) kwa ajili ya kusambaza umeme ndani ya  visiwa  118 vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchi nzima,ili kuwafikishia huduma za nishati ya umeme wananchi wote wanaoishi maeneo ya visiwa na yale ambayo siyo rahisi kufikiwa na gridi ya Taifa.

Mkurugenzi wa teknolojia ya Nishati jadidifu mbadala  kutoka REA  mhandisi Advera Mwijage ameeleza  hayo wakati wa ziara ya bodi ya wakurugenzi wa wakara hiyo walipotembelea moja ya kisiwa ambacho kiko kati ya visiwa 118 vinavyotakiwa kupitiwa mradi huo na kuongea na wananchi kisha kukagua maendeleo ya mradi.

Bodi ikiongozwa na Mwenyekiti wake balozi meja jenerali mstaafu Jacob Kingu  jana ilitembekea katika kisiwa Cha Musira  kilichopo ndani ya ziwa Viktoria Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera  ambapo ni moja ya kisiwa kilichotengewa zaidi ya shl.bil. 2 na serikali ili kupeleka nishati katika eneo hilo.

Mhandisi Mwijage amewaeleza wananchi wa Musira  kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mkataba na banki ya dunia ili kuwezesha upatikanaji wa nishati ambayo ni salama kwa Tanzania bara lakini  visiwani,ambapo Serikali ilipewa shl.bili.8 ili kuwafikishia wananchi  wa visiwa miundombinu ya umeme. 

"Sasa kulingana na jiografia ya visiwa vyetu ilivyo, mradi uliopendekezwa  ni wa kufunga mifumo ya umeme jua ambayo inafungwa kwenye kila kaya viswani na unalenga kufunga mifumo ipatayo 20 katika mikoa saba ikiwemo mkoa wa Kagera itagusa Wilaya 16 na kata 43 kati ya hizo nane ni za mkoa wa Kagera zilizoko Muleba na Manispaa ya Bukoba ambao unagharimu shl.bil.2.1"ameeleza Mwijage

Amesema kwanini Serikali imepeleka mradi wa umeme jua visiwani ni kutokana na ukweli kwamba maeneo hayo inakuwa vigumu sana kufikishwa miradi ya gridi ya Taifa sababu ya gharama kubwa pia wananchi wa meneo hayo wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu kwa kukosa nishati ya umeme hivyo mradi huo umeleta tija kwani utachochea maendeleo ya wananchi. 

"Miradi hiyo imefadiiliwa na Serikali kwa kiwango kifuatacho ambapo mifumo itakayofungwa ni kilowatts 50 ambayo inauzwa kwa shilingi 427,000 ambapo mwananchi atalipia 107,000  ,kilowatts 80 inauzwa kwa shl.515,000 na mwananchi atalipia shl 180,000 na kilowatt 100 inanunuliwa 700,000 na wananchi watalipia shl. 346,000  ambapo Serikali iliongeza fedha inayobaki.

Amesema Serikali imetambua umuhimu wa wananchi kupata huduma hii ndo maana imeweka ruzuku kubwa hivyo alitoa wito kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kujiepusha na vitendo vya rushwa kwani hakuna sababu ya wananchi kutoa rushwa ndipo wapelekewe mradi hilo siyo lengo la Serikali,

pia aliwashauri wananchi kuitunza miundombi hiyo ili wapate tija na maendeleo 

Aidha mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa REA  balozi Meja Jenerali mstaafu Jacob Kingu  amesema kuwa ujio wa umeme wa Nishati ya jua wanayofungiwa wananchi utachechemua shughuli za kiuchumi Kwa wakazi wa kisiwa Cha Musira na vingine 117 vilivyolengwa.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa REA  mhandisi Hasan Said  amewashauri wananchi kuchangamkia fursa hiyo katika kujiletea maendeleo.

Baadhi ya wananchi ambao tayari wameanza kunufaika na mpango huo wa serikali wa kuwafungia nishati ya umeme wa jua licha ya kuishukuru serikali wameelezea matarajio na tija waliyopita baada ya kufungiwa.

Stela Petro amesema kabla ya  kufikiwa na mradi huo alikuwa akivuka ng'ambo ya pili kuongeza umeme kwenye simu,alikuwa akifunga biashara yake mapema ata kuamka kufungua biashara yake mapema ililiwa ngumu.

"Baada ya kufungiwa umeme nimeweza kuchaji simu kwangu,tunaweza kuchaji taa zetu zinazotumika katika uvuvi kirahisi kuliko olivyokuwa nyuma na anaweza kufanyabiashara zake za kuuza vinywaji na chakula mpaka usiku wakati alikuwa akifunga saa 12 jioni hivyo nimeongeza wateja na kipatao kuongezeka kutoka shil.30,000 hadi 60,000 kwa siku"anasema Stela.

Kamishna wa Nishati kutoka wizara ya Nishati Styden Rebangira amesema kuwa serikali umeamua kupeleka nishati ya jua kutokana na kupunguza gharama za usafirishaji wa umeme kuwa kubwa hivyo imekuja na mradi wa gharama nafuu.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top