Skip to main content

Posts

Showing posts from November 21, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT. MWIGULU ASEMA MIGOGORO YA ARDHI ISICHOCHEE VISASI*

  *_▪ Aonya dhidi ya kujichukulia sheria mikononi na kuuza ardhi kinyemela_* *_▪ Serikali yakamilisha usanifu wa barabara ya njia sita kutoka Picha ya Ndege hadi Chalinze_* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekemea tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi na kuonya kuwa Serikali haiungi mkono uvunjaji wa sheria wa makusudi. “Tusiruhusu uvunjifu wa sheria wa makusudi kwa sababu utaua udugu wetu uliokuwepo kwa miaka mingi. Lazima tuzingatie utawala wa sheria, tuache utaratibu wa uvunjifu wa sheria na kujichukulia sheria mkononi,” amesisitiza. Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Polisi, wilayani Chalinze, mkoani Pwani, jana jioni (Jumamosi, Novemba 21, 2026), Waziri Mkuu alisema mmomonyoko wa utawala wa sheria unaalika visasi na makovu yasiyopona. “Tusibaguane au kuchukiana kwa sababu ya ardhi kwani yenyewe haiongezeki lakini mahitaji ya ardhi yanaongezeka. Tunatakiwa tuweke nguvu kubwa katika kupanga matumizi bora ya ardhi na tuheshimu ...