Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Ndejembi awasili Ethiopia kushiriki Mkutano wa Sekta ya Nishati

 Waziri Ndejembi awasili Ethiopia kushiriki Mkutano wa Sekta ya Nishati  WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Disemba 09, 2025 amewasili jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Mawaziri wa sekta ya nishati wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wenye lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kuendeleza matumizi bora ya nishati kwa Bara la Afrika.  Kongamano hilo litafanyika jijini Addis Ababa kwa siku mbili ambapo litahusisha pia Nchi hizo wanachama wa AU kubadilishana uzoefu katika mikakati, mipango, changamoto na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza ya miradi ya kuongeza ufanisi wa nishati katika bara la Afrika Katika kongamano hilo pia Mkakati na Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati barani Afrika utazinduliwa ambao unaendana na malengo ya Mpango wa Afrika wa Mwaka 1963.  Aidha kongamano hilo la siku mbili limetanguliwa na mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya Nishati katika kuwajengea uzoefu kwenye maeneo ya kupunguza Ma...

Jeshi la Polisi lasema hali ni shwali nchi nzima

Hali ni shwali Tanzania, Wananchi wapongeza vyombo vya ulinzi

Mpotoshaji kuhusu Graphite apingwa

Wadau Wavunja Ukimya, Wafafanua Ukweli wa Mradi Mkakati wa Mahenge** Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam Mjadala kuhusu mradi wa kimkakati wa Mahenge Graphite umechukua sura mpya baada ya wachambuzi wa masuala ya uchumi na wadau wa sekta ya madini kumjibu vikali mwanaharakati wa kisiasa, Martin Maranja Masese, wakimtuhumu kusambaza taarifa zisizo sahihi kuhusu mazungumzo ya Rais Samia Suluhu Hassan na Kaimu Balozi wa Marekani, Andrew Lentz. Kwa mujibu wa uchambuzi huo, madai ya Masese yameelezwa kama “propaganda za mtandaoni zilizokosa msingi wa kisheria na kiuchumi.”   *DAI LA “MGODI KUUZWA KWA USD 300 MILIONI” LAVUNJWA VIPANDE VIPANDE* Katika chapisho lake, Masese alidai kuwa Tanzania “imewauzia Wamarekani mgodi wa graphite kwa dola milioni 300”. Lakini taarifa rasmi zinaeleza wazi kuwa: • USD milioni 300 si bei ya mgodi, bali ni makadirio ya uwekezaji (CAPEX) wa kampuni ya ubia Faru Graphite Corporation (FGC) inayomilikiwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na kampuni ya Austra...

Waziri wa Ulinzi na JKT Mhe Dkt Rhimo Simeon Nyansaho ametembelea Makao Makuu ya Jeshi la kujenga Taifa

Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho (mb) tarehe 8 Desemba 2025, amefanya ziara ya kikazi kwa makao makuu ya kujenga Taifa, chamwino mkoani Dodoma. Ziara hiyo ya waziri wa ulinzi ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi alizozianza kwa ajili ya kujitambulisha na Maafisa, askari, watumishi wa umma wa wizara ya Ulinzi.  Mara baada ya kuwasili MMJKT, Mhe.Dkt.Rhimo Simeon Nyansaho alipokelewa na mwenyeji wake mkuu wa JKT, Meja jenerali Rajabu Mabele na uongozi mzima wa Jeshi la kujenga Taifa.  Pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo waziri wa ulinzi na JKT alipata wasaa wa kupanda mti wa kumbukumbu na baadae shughuli na Maafisa, askari na watumishi wa umma wa wizara.  Katika hotuba yake waziri wa ulinzi na JKT Mhe.Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho amempongeza mkuu wa JKT kwa mapokezi mazuri na kusema pia serikali kupitia wizara anayoiongoza ataendelea kuiwezesha JKT ili itekeleze majukumu yake ya msingi ambayo ni malezi ya vijana, Mali na u...

Prof Kitila Aelezea Mafanikio na Mipango Mikubwa Chini ya Rais Samia

 Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo amesema serikali imefanikisha kuongezeka kwa idadi ya miradi ya uwekezani katika miaka mitano iliyopita kutoka miradi 252 hadi miradi 901, kutoka mwaka 2021 hadi mwaka 2024 ikiwa ni sambamba na ongezeko la mitaji kutoka dola bilioni 3.7 kwa mwaka 2021 hadi kufikia dola bilioni 9.3 kwa mwaka 2024. Akizungumza mapema hii leo Disema 8, 2025, Waziri Mkumbo , katika hafla ya mkutano wa mawaziri na waandishi wa vyombo vya habari katika ofisi ya kituo cha ukombozi kilichopo jijini Dar es salaam ambapo pia amesema serikali imeandaa hekta elfu 78,444 mashamba ya jumla huku mashamba kutoka taasisi za serikali ni zaidi ya mashamba 212. Aidha, waziri Kitila amesema kuwa serikali inatarajia kuzindua kituo cha kuhudumia wawekezaji vijana katika taifa, lengo likiwa ni kuwapatia uzoezi katika maswala ya uwekezaji na ufanyaji wa biashara ambapo pia itasaidia kuchochea kasi ya wawekezaji vijana nchini. Katika kutambua hilo serikal...