Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho (mb) tarehe 8 Desemba 2025, amefanya ziara ya kikazi kwa makao makuu ya kujenga Taifa, chamwino mkoani Dodoma.
Ziara hiyo ya waziri wa ulinzi ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi alizozianza kwa ajili ya kujitambulisha na Maafisa, askari, watumishi wa umma wa wizara ya Ulinzi.
Mara baada ya kuwasili MMJKT, Mhe.Dkt.Rhimo Simeon Nyansaho alipokelewa na mwenyeji wake mkuu wa JKT, Meja jenerali Rajabu Mabele na uongozi mzima wa Jeshi la kujenga Taifa.
Pamoja na mambo mengine katika ziara hiyo waziri wa ulinzi na JKT alipata wasaa wa kupanda mti wa kumbukumbu na baadae shughuli na Maafisa, askari na watumishi wa umma wa wizara.
Katika hotuba yake waziri wa ulinzi na JKT Mhe.Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho amempongeza mkuu wa JKT kwa mapokezi mazuri na kusema pia serikali kupitia wizara anayoiongoza ataendelea kuiwezesha JKT ili itekeleze majukumu yake ya msingi ambayo ni malezi ya vijana, Mali na ulinzi wa Taifa kwa ujumla.







