Prof Kitila Aelezea Mafanikio na Mipango Mikubwa Chini ya Rais Samia

GEORGE MARATO TV
0


 Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo amesema serikali imefanikisha kuongezeka kwa idadi ya miradi ya uwekezani katika miaka mitano iliyopita kutoka miradi 252 hadi miradi 901, kutoka mwaka 2021 hadi mwaka 2024 ikiwa ni sambamba na ongezeko la mitaji kutoka dola bilioni 3.7 kwa mwaka 2021 hadi kufikia dola bilioni 9.3 kwa mwaka 2024.

Akizungumza mapema hii leo Disema 8, 2025, Waziri Mkumbo , katika hafla ya mkutano wa mawaziri na waandishi wa vyombo vya habari katika ofisi ya kituo cha ukombozi kilichopo jijini Dar es salaam ambapo pia amesema serikali imeandaa hekta elfu 78,444 mashamba ya jumla huku mashamba kutoka taasisi za serikali ni zaidi ya mashamba 212.

Aidha, waziri Kitila amesema kuwa serikali inatarajia kuzindua kituo cha kuhudumia wawekezaji vijana katika taifa, lengo likiwa ni kuwapatia uzoezi katika maswala ya uwekezaji na ufanyaji wa biashara ambapo pia itasaidia kuchochea kasi ya wawekezaji vijana nchini.

Katika kutambua hilo serikali imekusudia kufungua ofisi za kisekta katika mikoa yote nchini ili kuweza kusaidia kutoa huduma za kiuwekezaji katika taifa ili kuwarahisishia vijana kupata huduma za kiuwekezaji.

Sambamba na hilo serikali imekusudia kubuni na kuanzisha vivutio vipya kqtika uwekezaji ambavyo ni vya kikodi na visivyo kuwa vya kikodi ili kusaidia wawekezaji.

Hata hivyo waziri mkumbo amesema serikali kupitia wizara ya mipango na uwekezaji inapanga kuwa kutanisha wawekezaji na wizara mbalimbali katika kila baada ya miezi mitqtu lengo likiwa ni kuwasikiliza na kutatua changamoto za wawekezaji.

Katika kuongeza mzunguko wa wa wawekezaji serikali inapanga kuweka kipaumbele katika utazingatia kilimo katika uchakataji wa mazao ya kilimo pamoja na bidhaa mbalimbali kutoka nje ambazo zitaweza kuokoa takribani trilioni 2.5 za kitanzania.

Waziri Mkumbo pia amesema kuwa serikali katika mpango wake kupitia dira ya taifa itaenda kuweka mpango wa kuboresha miji yote nchi nq kuboresha miundombinu ili kuvutia mji na kuhamasisha utalii.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top