Waziri Ndejembi awasili Ethiopia kushiriki Mkutano wa Sekta ya Nishati

GEORGE MARATO TV
0

 Waziri Ndejembi awasili Ethiopia kushiriki Mkutano wa Sekta ya Nishati 


WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Disemba 09, 2025 amewasili jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Mawaziri wa sekta ya nishati wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wenye lengo la kujadili na kuweka mikakati ya kuendeleza matumizi bora ya nishati kwa Bara la Afrika. 

Kongamano hilo litafanyika jijini Addis Ababa kwa siku mbili ambapo litahusisha pia Nchi hizo wanachama wa AU kubadilishana uzoefu katika mikakati, mipango, changamoto na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza ya miradi ya kuongeza ufanisi wa nishati katika bara la Afrika


Katika kongamano hilo pia Mkakati na Mpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati barani Afrika utazinduliwa ambao unaendana na malengo ya Mpango wa Afrika wa Mwaka 1963. 

Aidha kongamano hilo la siku mbili limetanguliwa na mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya Nishati katika kuwajengea uzoefu kwenye maeneo ya kupunguza Matumizi ya umeme katika sekta za majengo, viwanda, usafiri pamoja na majumbani.

Mhe Waziri Ndejembi ameongozana na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga ambapo amepokelewa na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) na Kamisheni ya Uchumi Afrika (UNECA), Mhe. Innocent Shiyo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top