Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri wa Ulinzi na Jkt aongoza Mazishi ya Mkuu wa Jkt Mstaafu

 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Stargomena Lawrence Tax ameongoza Maafisa, Askari, vijana wa JKT, watumishi wa umma na waombolezaji katika mazishi ya  marehemu Meja Jenerali Martine Busungu (Mstaafu) yaliyofanyika Kijiji cha Luchelele Jijini Mwanza tarehe 28 Disemba 2024.  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda katika mazishi hayo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajab Nduku  Mabere amesema, Meja Jenerali Busungu (Mstaafu) akiwa mtumishi ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania amelitumikia jeshi kwa kipindi cha miaka thelathini na nne (34), ambapo alikuwa mwaminifu, mtiifu Hodari katika kutekeleza majukumu yake. Meja Jenerali Busungu Mstaafu) alifariki dunia tarehe 24 Disemba 2024 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam

Huu Ni Upendo Mkubwa Wa Mbunge Wa Ilala Mh Zungu

 Zungu amefika kutoa salamu za pole kwa Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kariakoo Kaskazini Ndg. Mwinyi Ludete nyumbani kwao Mtoni Kijichi, aliepatwa na msiba wa kuondokewa na Dada yake.   Zungu anatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu. Innalilah wa Innalilah Rajoun

Oparesheni Ya Polisi Kagera Yakamata 15 Wakiwemo Wa Mauaji

 Na Angela Sebastian; Bukoba  Jeshi la polosi mkoani Kagera linawashikilia watutuhumiwa 15 wa matukio mbalimbali ikiwemo wawili wa mauaji ya Editha Anderson (32) kutokana na operesheni iliyofanyika kwa siku mbili maeneo mbambali ya mkoa huu. Kamanda wa polisi mkoani humo Blasius Chatanda aliwataja watuhumiwa hao kuwa Answari Mutalemwa (25) na Kenedi Muganyizi (25) wakazi wa mtaa wa Kashenye kata ya Kashai ambapo wanatuhumiwa kwa kosa na kumuua Editha Anderson (32) aliyekuwa Mkazi wa mtaa wa Kilimahewa kutokana na wivu wa kimapenzi. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda Chatanda alisema kuwa watuhumiwa hao walitekeleza mauaji hayo mnamo Desemba 12 mwaka huu baada ya Answari Mutalemwa kubaini Editha Anderson ambaye alikuwa mpenzi wake kuwa kwenye mahusiano na mtu mwingine. "Baada ya Mutalemwa kubaini kuwa mpezi wake huyo aliyekuwa mke wa mtu mwingine,alikuwa tena mchupuko wa kijana mwingine tena aliyekuwa akifanya kazi na Editha ndipo alipata wivu na kisha kushirikiana na...

Wananchi Musoma Wafurahia offer ya Muwasa kurejeshewa Maji bila Faini

  Na Shomari Binda-Musoma WANANCHI Wilaya ya Musoma wameshukuru na kufurahia nafuu ya kurejeshewa huduma ya maji iliyotolewa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Musoma " MUWASA". Wakizungumza na GMTV wananchi waliositishiwa huduma hiyo wamesema nafuu iliyotolewa itawafanya kurejesha maji na kuendelea na huduma. Tatu Juma mkazi wa Majita Road ambaye kwa muda amesitishiwa huduma kutoka na kushindwa kulipa kwa muda amesema anakwenda ofisi za MUWASA kukamilisha taratibu. Amesema deni lake limekuwa kubwa kutokana na changamoto mbalimbali ambazo zilipelekea kushindwa kulipa kwa wakati. Tatu amesema tangazo lililotolewa na MUWASA kuhusu kurejeshewa huduma ya maji bila faini na kuingia mkataba   wa kulipa taratibu amelisikia na anakwenda kukamilisha taratibu. " Niwashukuru sana MUWASA kwa utaratibu walioutoa ambao unakwenda kutusaidia kurejesha maji. " Maji ni huduma muhimu kuwepo nyumbani na hiki ambacho wamekifanya MUWASA tunasema nj asante kwao",amesema. Mkurug...

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka Siku tatu baada ya Ukaguzi Kubaini haina hitilafu-Sebukoto

Kampuni ya Meli Tanzania(TASHICO)imetoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la kupinduka kwa meli ya Mv.Serengeti lililotokea usiku wa kuamkia Desemba 26 mwaka huu katika Bandari ya Mwanza Kusini. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Paul Sebukoto amesema kuwa Meli hiyo imelalia upande wa nyuma baada ya maji kuingia ndani. ‘’Meli hii ilikuwa kwenye eneo la Maegesho,Maji yameingia ndani zikiwa zimepita kama siku mbili au tatu baada ya kufanyiwa ukaguzi uliobaini iko sawa,kwa hiyo ni lazima kutakuwa na chanzo ambacho kimesababisha maji kuingia ndani ya meli na kuipeleka chini upande wa nyuma’’alisema Sebukoto na Kuongeza kuwa ‘’Sasa tofauti na Tafsiri kuwa meli imepinduka au imezama ni kwamba meli hii haijapinduka wala haijazama isipokuwa tunasema imeegemea upande wa nyuma baada ya kulemewa na maji yaliyoingia ndani’’ Sebukoto amesema kuwa shughuli zinazofanyika kwa sasa ni kuinyanyua Meli hiyo kwa nyuma ili iweze kurudi kwenye hali yake ya...

Mnadhimu wa Jwtz aongoza Maafisa,Askari na wananchi kuaga mwili wa Meja Jenerali Mstaafu Busungu

  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman, ameongoza Maafisa, Askari na Waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Meja Jenerali Martin Busungu, katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.  Marehemu Meja Jenerali Martin Busungu, enzi za uhai wake alishika nafasi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) kuanzia mwaka 2018 hadi 2019. Marehemu Meja Jenerali Martin Busungu, alifariki dunia tarehe 24 Desemba 2024, katika hospitali ya Taifa ya Rufaa Muhimbili Dar es Salaam na kuagwa leo tarehe 27 Desemba 2024 na kusafarishwa kuelekea Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika Nyegezi, Mwanza tarehe 28 Desemba 2024.