Oparesheni Ya Polisi Kagera Yakamata 15 Wakiwemo Wa Mauaji

GEORGE MARATO TV
0


 Na Angela Sebastian; Bukoba 

Jeshi la polosi mkoani Kagera linawashikilia watutuhumiwa 15 wa matukio mbalimbali ikiwemo wawili wa mauaji ya Editha Anderson (32) kutokana na operesheni iliyofanyika kwa siku mbili maeneo mbambali ya mkoa huu.

Kamanda wa polisi mkoani humo Blasius Chatanda aliwataja watuhumiwa hao kuwa Answari Mutalemwa (25) na Kenedi Muganyizi (25) wakazi wa mtaa wa Kashenye kata ya Kashai ambapo wanatuhumiwa kwa kosa na kumuua Editha Anderson (32) aliyekuwa Mkazi wa mtaa wa Kilimahewa kutokana na wivu wa kimapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda Chatanda alisema kuwa watuhumiwa hao walitekeleza mauaji hayo mnamo Desemba 12 mwaka huu baada ya Answari Mutalemwa kubaini Editha Anderson ambaye alikuwa mpenzi wake kuwa kwenye mahusiano na mtu mwingine.

"Baada ya Mutalemwa kubaini kuwa mpezi wake huyo aliyekuwa mke wa mtu mwingine,alikuwa tena mchupuko wa kijana mwingine tena aliyekuwa akifanya kazi na Editha ndipo alipata wivu na kisha kushirikiana na Muganyizi na kumuua kwa kumnyonga na mtandio kisha kuficha simu yake na kuizima isipatikane hewani"alieleza kamanda 

Sambamba na hilo jeshi hilo linamshikilia Jafesi Rusole(52)mkulima mkazi wa kijiji cha Kakindo kata ya Kyebitembe Wilayani Muleba kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya Gobore pamoja na nyaraka za Serikali.

Wakati huo huo katika kuimalisha usalama wa mkoani humo Decemba 25 mwaka huu jeshi la polisi lilifanya msako mkali katika maeneo yote ambapo katika maeneo ya Rwagati kata Kemondo walikamata watu watatu kwa tuhuma za wizi wa mashine za kuendesha boti(Enginer Boat) zipatazo saba ambapo moja imetambuliwa kuibiwa kutoka nchi Uganda, mitumbwi miwili na nyavu 184 ambazo zilizoibiwa kwa wavuvi sehemu mbalimbali.

Kamanda hakutaja majina ya watuhumiwa hao kwasababu za upelelezi ambao bado unaendelea ili kuwabaini wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Pia jeshi hilo Decemba 27 mwaka huu liliendelea kufanya operesheni katika barabara kuu kutoka Manispaa ya Bukoba hadi Nyakanazi Wilayani Biharamulo na barabara nyingine zinazokwenda vijijini ili kuhakikisha wananchi wanasafiri salama kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Alisema katika operesheni hiyo jumla ya madereva tisa walikamatwa kwa makosa ya kuendesha gari wakiwa wamelewa na mwendo kasi na wote wamefungiwa leseni zao.na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top