Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Paul Sebukoto amesema kuwa Meli hiyo imelalia upande wa nyuma baada ya maji kuingia ndani.
‘’Meli hii ilikuwa kwenye eneo la Maegesho,Maji yameingia ndani zikiwa zimepita kama siku mbili au tatu baada ya kufanyiwa ukaguzi uliobaini iko sawa,kwa hiyo ni lazima kutakuwa na chanzo ambacho kimesababisha maji kuingia ndani ya meli na kuipeleka chini upande wa nyuma’’alisema Sebukoto na Kuongeza kuwa
‘’Sasa tofauti na Tafsiri kuwa meli imepinduka au imezama ni kwamba meli hii haijapinduka wala haijazama isipokuwa tunasema imeegemea upande wa nyuma baada ya kulemewa na maji yaliyoingia ndani’’
Sebukoto amesema kuwa shughuli zinazofanyika kwa sasa ni kuinyanyua Meli hiyo kwa nyuma ili iweze kurudi kwenye hali yake ya kawaida na kuondoa yale maji sanjari na kutafuta chanzo kilichosababisha maji kuingia ya Meli.
‘’Mpaka sasa hatujajua sababu za meli hii kuegemea upande wa nyuma na kwanini maji yameingia ndani,ni mpaka hapo wataalam watakapoirudisha katika hali yake ya kawaida ndipo sasa ipandishwe kwenye chelezo kwa ajili ya kukaguliwa mwili wake wote,hapo ndo tutaweza kutoa taarifa sahihi kuhusu chanzo ’’alisema Sebukoto
Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tashico amesema kuwa kipaumbele cha kampuni hiyo ni kuimarisha usalama wa vyombo vyake vinavyotoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo pamoja na vilivyoegeshwa kwenye bandari Mwanza kusini.
‘’Changamoto za namna hii zinapojitokeza ni sehemu ya kutufanya sisi tuzidishe usalama kuliko ilivyokuwa,Tunajali usalama na tunajitahidi kufuata hatua zote za kiusalama kama inavyotakiwa na sheria za usafirishaji kwa njia ya maji,Ninachoweza kusema hapa ni kuwa tutazidisha kuweka usalama zaidi ikiwemo kutumia njia za kisasa kama kufunga kamera pamoja na kuweka mifumo ya kiusalama ikiwemo alarm.Hizi meli zetu zimetengenezwa zamani,ile mifumo ya kisasa kama maji yameingia ndani ya meli au moshi haikuwepo lakini tunavyoenda kwenye matengenezo na marekebisho sasa hivi tutahakikisha kwamba ile mifumo ya kisasa inakuwa sehemu ya marekebisho ya meli zetu ili kufanya haya matukio ya Kupinduka na Kuzama kuwa historia’’alisema Sebukoto
Meli ya MV.Serengeti imesitisha huduma za uchukuzi wa abiria na mizigo katika ziwa victoria tangu mwaka 2016 na Tangu kipindi hicho ilikuwa imeegeshwa kwenye bandari ya mwanza kusini kwa ajili ya kusubiri kufanyiwa matengenezo makubwa.
Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika bandari ya mwanza kusini ikiwa ni miezi michache tangu meli nyingine ya Mv.Clarius kupinduka na kuzama katika bandari ya Mwanza Kaskazini
Meli ya Mv.Clarius ilipinduka na kuzama Usiku kuamkia mei 19 Mwaka huu ikiwa kwenye eneo la maegesho ya bandari ya mwanza Kaskazini.
Zaidi ya miezi Saba tangu kutokea kwa Tukio hilo,hakuna Taarifa zozote za uchunguzi zilizotolewa kwa umma licha ya Mamlaka inayosimamia usafiri wa majini Nchini(TASAC) kuahidi kufanya hivyo.