Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Stargomena Lawrence Tax ameongoza Maafisa, Askari, vijana wa JKT, watumishi wa umma na waombolezaji katika mazishi ya marehemu Meja Jenerali Martine Busungu (Mstaafu) yaliyofanyika Kijiji cha Luchelele Jijini Mwanza tarehe 28 Disemba 2024.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda katika mazishi hayo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajab Nduku Mabere amesema, Meja Jenerali Busungu (Mstaafu) akiwa mtumishi ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania amelitumikia jeshi kwa kipindi cha miaka thelathini na nne (34), ambapo alikuwa mwaminifu, mtiifu Hodari katika kutekeleza majukumu yake.
Meja Jenerali Busungu Mstaafu) alifariki dunia tarehe 24 Disemba 2024 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam