Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda ashinda kesi ya Kulawiti

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt.Yahaya Nawanda katika Kesi ya kumwingilia kinyume na Maumbile Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine  iliyokuwa ikimkabili. Uamuzi huo wa kesi namba 1883/2024 umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Erick Marley baada ya kujiridhisha kuwa hakukuwa na ushahidi unaoweza kumtia hatiani Dkt.Nawanda Hakimu Mkazi Mfawidhi Marley amesema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri umeacha shaka katika maeneo mbalimbali ikiwemo Video Mjongeo(CCTV)zilizowasilishwa kutoonyesha sehemu wawili hao walikuwa kwenye gari wakitenda tukio hilo. Jamhuri kutowasilisha vipimo vya vinasaba(DNA)vilivyochukuliwa kwa wawili hao huku katika ushahidi wake Binti aliyedai kulawitiwa na Dkt.Nawanda akidai kufanyiwa ukatili huo kwenye gari nyeupe lakini gari hilo halikuwa nyeupe bali ya Silver. Aidha binti huyo alisema wakati anafanyiwa kitendo hicho,gari lilikuwa na vioo(Tinted)na nje haku...

Waziri Kikwete:Fursa za ajira kwa Vijana nje ya nchi Kipaumbele cha Serikali ya Rais Samia

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kufungua fursa zaidi za ajira kwa watanzania nje ya nchi.  Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema serikali inatekeleza mpango wa kuwaandaa vijana kuwa na ujuzi stahiki unao wawezesha kumudu ushindani kwenye soko la ajira la kimataifa sambamba na kufanya kazi zenye tija.  Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Novemba 28, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwaaga Vijana wa Kitanzania wanaoenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia.  Waziri Ridhiwani Kikwete, amebainisha kuwa Serikali imesaini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya ajira na nchi ya Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, Iran na Qatar kwa lengo la kuongeza fursa zaajira kwa watanzania kwenye nchi hizo. "Serikali imeweka malengo mahususi ya kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania kutoka 556,065 kwa mwaka 2022 hadi 1,00...

Naibu Waziri Sangu Apiga Kura, Awaomba Wananchi Kwela Kuendelea Kuwa Watulivu

  Na Mwandishi Wetu-Rukwa WANANCHI wa Jimbo la Kwela wametakiwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua viongozi Bora watakao waongoza kwa amani,usala na utulivu. Pia amesisitiza kuwa uchaguzi huo ni fursa kwa wananchi kupata viongozi wa karibu wanaojua changamoto zinazowakabili za moja kwa moja katika maeneo yao. Naibu Waziri, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ma Utawala Bora Mhe.Deus Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Kwela ametoa kauli hiyo  mapema leo Jumatano Novemba 27, 2024 mara  baada ya kumaliza kupiga kura katika Kitongoji cha Pokopoko Kata ya Laela Mkoani Rukwa  "Niwazi nimeridhika na idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika kitongoji hichi na jinsi mchakato wa uchaguzi unavyoendelea, ," Amesema Na kuongeza"Niwaombe Wananchi waliobaki kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kupiga kura,"Amesema  Hata hivyo amesisitiza kuwa,ushiriki wa kila raia ni muhimu katika kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanikiwa kwa haki na uwazi...

Rc Mtambi Awataka Wananchi Mkoa wa Mara Kuendelea Kudumisha Demokrasia

 Ghati Msamba- Musoma MKUU wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amewataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kudumisha demokrasia kama walivyofanya katika zoezi la uandikishaji, na kuhakikisha wanakamilisha zoezi la upigaji kura kwa uangalifu na kwa kufuata sheria. Akizungumza baada ya kupiga kura katika Kituo cha Ofisi ya Kata ya Mukendo, Mtambi alisisitiza umuhimu wa kuepuka vitendo vya kupiga kura mara mbili na kufanya kampeni katika vituo vya kupigia kura. Alisema wananchi wanapaswa kuhakikisha wanarudi nyumbani mara baada ya kupiga kura, na kuepuka kurudi tena kwenye vituo vya kupigia kura, kwani hilo ni kinyume cha sheria. "Kwa sasa tayari mimi nimepiga kura, naomba wananchi wote mliojiandikisha mkaendelee na zoezi hili ili tuweze kupata viongozi wa serikali za mitaa watakaoshirikiana nasi katika kuleta maendeleo," alisema Mtambi. Mkuu huyo wa Mkoa pia aliwapongeza wananchi wa Mara kwa kujitokeza kwa wingi na kudumisha demokrasia, akisisitiza kuwa haki ya kila mmoja ni kum...

Mhe.Mathayo apiga kura Kituo cha Kupigia Kura Sido

Mbunge wa Jimbo la Musoma mjini Mhe Vedastus Mathayo Leo 27/11/2024 amepiga yake katika kituo cha kupigia kura Sido kilichopo mtaa wa Baruti, kata ya Nyakato.  Mhe Mathayo ameongozana na mwenza wake Bi Elizabeth Vedastus Mathayo.  Akizungumzia zoezi zima la upigaji kura, Mhe Mathayo amesema ametembelea baadhi ya maeneo, zoezi hilo linaenda vizuri

Mama Mary Majaliwa akiwa kwenye Foleni ya Kupiga Kura

Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akiweka Kura yake katika sanduku kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji kwenye kituo cha Shule ya Msingi Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi,  Novemba 27, 2024.