Na Mwandishi Wetu-Rukwa
WANANCHI wa Jimbo la Kwela wametakiwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchagua viongozi Bora watakao waongoza kwa amani,usala na utulivu.
Pia amesisitiza kuwa uchaguzi huo ni fursa kwa wananchi kupata viongozi wa karibu wanaojua changamoto zinazowakabili za moja kwa moja katika maeneo yao.
Naibu Waziri, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ma Utawala Bora Mhe.Deus Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Kwela ametoa kauli hiyo mapema leo Jumatano Novemba 27, 2024 mara baada ya kumaliza kupiga kura katika Kitongoji cha Pokopoko Kata ya Laela Mkoani Rukwa
"Niwazi nimeridhika na idadi ya wapiga kura waliojitokeza katika kitongoji hichi na jinsi mchakato wa uchaguzi unavyoendelea, ," Amesema
Na kuongeza"Niwaombe Wananchi waliobaki kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kupiga kura,"Amesema
Hata hivyo amesisitiza kuwa,ushiriki wa kila raia ni muhimu katika kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanikiwa kwa haki na uwazi, huku akiwapongeza wale ambao tayari wamepiga kura kwa kuwa mfano mzuri wa uzalendo.