Uamuzi huo wa kesi namba 1883/2024 umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Erick Marley baada ya kujiridhisha kuwa hakukuwa na ushahidi unaoweza kumtia hatiani Dkt.Nawanda
Hakimu Mkazi Mfawidhi Marley amesema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri umeacha shaka katika maeneo mbalimbali ikiwemo Video Mjongeo(CCTV)zilizowasilishwa kutoonyesha sehemu wawili hao walikuwa kwenye gari wakitenda tukio hilo.
Jamhuri kutowasilisha vipimo vya vinasaba(DNA)vilivyochukuliwa kwa wawili hao huku katika ushahidi wake Binti aliyedai kulawitiwa na Dkt.Nawanda akidai kufanyiwa ukatili huo kwenye gari nyeupe lakini gari hilo halikuwa nyeupe bali ya Silver.
Aidha binti huyo alisema wakati anafanyiwa kitendo hicho,gari lilikuwa na vioo(Tinted)na nje hakukuwa na watu waliokuwa wanapita lakini video iliyowasilishwa zilizonesha gari hilo halikuwa Tinted na pia watu walikuwa wakipita nje na kuendelea na shughuli zao.
Awali Dkt.Nawanda alidaiwa kutenda kosa la kumwingilia Kinyume na Maumbile Juni pili Mwaka huu,Majira ya saa mbili unusu za Usiku kwenye eneo la Maegesho ya Magari ya baa ya The Cask iliyopo Jijini Mwanza