Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Takukuru Kagera Yabaini Mapungufu Miradi 10 ya Maendeleo

Na Angela Sebastian  TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Kagera imefanya ufatiliaji katika miradi ya maendeleo 18 yenye thamaniya shilingi billion 144.9 na kubaini miradi 10 yenye thamani ya shl biln 3.137 kuwa na mapungufu. Ezekia Sinkala ni Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera ameeleza hayo leo wakati akitoa taarifa yq utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ofisini kwake mjini Bukoba.  Senkala ametaja miradi iliyofuatiliwa kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya maji,ujenzi za wodi ya hospitali,ujenzi wa miundombinu ya barabara,ujenzi wa vyumba vya madarasa,shule za sekondari, ujenzi wa mabweni ya Sekondari. Anasema ufuatiliaji huo ulilenga kuhakikisha kuwa miradi yote inayotekelezwa inaendana na thamani ya fedha iliyotumika (Vulue for money) ambapo wameshauri wasimamizi wa miradi hiyo kufanyia kazi mapungufu hayo . Pia kwa kipindi hicho wamepokea jumla ya malalamiko 155 kati y...

EWURA CCC Yatoa Elimu Kwa Wanachuo na Watumishi wa COTC

Fresha Kinasa-Mara. KATIKA kutekeleza majukumu yake Ofisi ya Baraza la Ushauri la  Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) Mkoa wa Mara limetoa elimu juu ya utumiaji wa Huduma hizo kwa Watumishi 30  na   Wanafunzi wa Chuo Cha Afisa Tabibu 250  (COTC) kilichopo  Manispaa ya Musoma Mkoani humo.  Elimu hiyo imetolewa  Novemba 14, 2024 Chuoni hapo na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mkoa wa Mara Rhobinson Wangaso na wenzake  ikiwa ni moja ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo la kuyafikia makundi mbalimbali kuyaelimisha juu ya matumizi sahihi ya huduma hizo. Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo Wangaso amewaambia kuwa,   Watumiaji wa Huduma hizo wanalojukumu la kuhakikisha wanatumia huduma hizo kwa usahihi na kuzingatia wajibu wao  pamoja na  haki zao.  Amesema, Mtumiaji wa Huduma za Nishati ni maji ni Mtu yeyote, kampuni ama taasisi inayotumia bidhaa zinazodhibitiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nisha...

Lema Ampongeza Rais Samia

  Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kanda ya Kaskazini, na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema ni matamanio na mpango wa CHADEMA kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 hivyo wanashukuru na kupongeza juhudi za Serikali kurejeshwa wagombea wa CHADEMA katika mitaa na vijiji mbalimbali nchini. Lema ameyasema hayo leo, Novemba 13, 2024, katika mkutano wa CHADEMA Arusha. Lema ameendelea kusema kwamba ni kweli CHADEMA hawajaweka wagombea sehemu nyingi nchini, hivyo wagombea wachache kupata nafasi ya wagombea wao kurudishwa ni hatua ya kupongezwa na ishara ya utawala bora na Samia ameweza kutimiza ahadi yake ya kuimarisha demokrasia nchini. CHADEMA wametoa pongezi hizo kufuatia maagizo ya Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mchengerwa kutoa muda zaidi wa kushughulikia malalamiko na kurudishwa kwa wagombea walioenguliwa kwa makosa madogo na waliokosa udhamini wa vyama vyao.

Aliyosema Waziri wa Madini Anthony Mavunde Katika Mahojiano Maalum na Crown Media Kupitia Kipindi cha Kasri la Kikeke

 *Kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2024* *Na Wizara ya Madini* *Ukiuza Madini Nje ya Soko wewe ni mtoroshaji* Tulikuwa na changamoto ya biashara ya Madini kabla ya mwaka 2017 ambapo ilifanyika kiholela kutokana na kukosekana kwa masoko ya madini. Hivi sasa biashara yote inafanyika sokoni, ukiuzia nje ya Soko wewe ni mtoroshaji unakiuka Sheria za nchi na kupoteza mapato ya Serikali. *Tozo kwenye uchimbaji mdogo* Nimefanya vikao na wadau mbalimbali kusikiliza hoja zao lengo ni kuangalia namna ya kutatua changamoto kwenye shughuli za uchimbaji mdogo wa madini na biashara ya madini. Hivi sasa kodi zote zinazolipwa Serikalini zimebaki asilimia 9.3 kutoka 38. Mrabaha ni asilimia 6, ada ya ukaguzi asilimia1, TRA asilimia 2 (withholding tax) na Service levy asilimia 0.3. Serikali imechukua hatua kubwa kusikiliza changamoto za wachimbaji wadogo, kodi inayokusanywa inasaidia kujenga nchi yetu. *Mkakati wa Kuongeza Thamani Madini Nchini* Kwenye hotuba...

Rc Mtambi Aagiza Kusitishwa Uchaguzi wa Viongozi wa Mgodi wa Irasanilo

  Na Ghati Msamba- Mara  Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amemuagiza Afisa Madini wa Mkoa huo, Amin Msuya, kusitisha uchaguzi wa viongozi wa mgodi wa Irasanilo, uliopo Buhemba, Wilaya ya Butiama, na kupitia upya kanuni na katiba ya Kikundi cha Wachimbaji Wadogo wa mgodi huo ndani ya siku 21. Ameyasema hayo kwenye kikao cha Wachimbaji Wadogo  na viongozi wao kilichofanyika katika ukumbi wa uwekezaji wa mkoa huo. Lengo la kikao hicho ni kutatua changamoto za migogoro iliyopo baina ya wachimbaji wadogo na viongozi ili kila mmoja wao apate misingi stahiki ya kiutawala. Amewataka pia wachimbaji kuachana na tabia za kujiwekea makundi ambayo hayatawasaidia lolote na badala yake wabadilike na waungane kwa pamoja ili waweze kujikuzia uchumi na kuendelea kusimamia shughuli za mgodi, ili viongozi waliokuwepo wapishe uchunguzi. "Nimefuatilia hiki Kikundi kingetulia mngekuwa mbali, na mngekuwa mmeishaanzisha mradi wa ujenzi wa hoteli kubwa ambayo ingeweza kuwa chanzo cha kuw...

Tanzania Kuungana na Dunia Usalama wa Afya Kimataifa

📌 Dkt. Biteko Ataja Jitihada za Serikali Kuboresha Ajenda ya Mpango wa Kimataifa wa Usalama wa Afya 📌 Dkt. Biteko Afungua Kongamano la 14 la CUHAS 📌 Dkt. Biteko Aipongeza CUHAS kwa Tafiti na Mchango wake katika Sekta ya Afya 📌 Wanasayansi Kuunganisha Afya ya Binadamu, Wanyama na Mazingira kwa Matokeo Bora ya Afya Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mwaka 2015, Tanzania iliunga mkono Ajenda ya Mpango wa Kimataifa wa Usalama wa Afya na kuharakisha utekelezaji wa Sheria za Afya za Kimataifa ili kuzuia magonjwa ya kuambukiza kusambaa kimataifa.  Kupitia tathimini ya pamoja ya mwaka 2023 matokeo ya maendeleo ya Tanzania katika suala hilo inaonyesha hatua kubwa ambapo mwaka 2016 imedhihirika  azma imara ya Serikali katika kutekeleza Sheria za Afya za Kimataifa kwa kutumia njia moja ikikubali uunganishaji wa afya ya binadamu, wanyama, na mazingira. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 13, 20...