Na Angela Sebastian
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Kagera imefanya ufatiliaji katika miradi ya maendeleo 18 yenye thamaniya shilingi billion 144.9 na kubaini miradi 10 yenye thamani ya shl biln 3.137 kuwa na mapungufu.
Ezekia Sinkala ni Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera ameeleza hayo leo wakati akitoa taarifa yq utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ofisini kwake mjini Bukoba.
Senkala ametaja miradi iliyofuatiliwa kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya maji,ujenzi za wodi ya hospitali,ujenzi wa miundombinu ya barabara,ujenzi wa vyumba vya madarasa,shule za sekondari, ujenzi wa mabweni ya Sekondari.
Anasema ufuatiliaji huo ulilenga kuhakikisha kuwa miradi yote inayotekelezwa inaendana na thamani ya fedha iliyotumika (Vulue for money) ambapo wameshauri wasimamizi wa miradi hiyo kufanyia kazi mapungufu hayo .
Pia kwa kipindi hicho wamepokea jumla ya malalamiko 155 kati ya hayo 65 yalihusu rushwa na kufunguliwa majalada ya uchunguzi.
Amesema kwa sasa tunapoelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa Takukuru wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaenda kutoa elimu kwa wananchi na makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa kisiasa lengo likiwa ni kuhakikisha uchaguzi unafanyika bila kuwepo vitendo vya rushwa.


