Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majiko Banifu kupunguza matumizi ya mkaa na kuni Mbeya

📌 *Majiko banifu 9,330 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Mbeya*  📌 *Wilaya Sita kunufaika na mradi*  📌 *Kila Wilaya pata majiko 1,555*  📍 *MBEYA*  Serikali ya Mkoa wa Mbeya kupitia Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu, Rodrick Mpogolo leo Jumanne Septemba 2, 2025 imepokea mradi wa kusimamia na matumizi ya majiko banifu 9,330 yenye ufanisi mkubwa katika utumiaji wake. Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya mradi Mhandisi wa miradi kutoka kwa nishaji vijijini (REA), Raya Majallah amesema, Kupitia utafiti 2016 unakadiria kuwa takribani watu 33,024 hufariki kabla ya kila mwaka huu ni sawa na asilimia 8.49 ya vifo vyote nchini Tanzania, kutokana na magonjwa ambayo yanachangiwa uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba ya upikaji kwa kutumia matumizi yasiyo safi na salama. Hivyo kwa kutambua hilo, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijiji imeaanda mpango wa kuamua na kuondoa majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku ili kupona athari za kiafya na mazingira zinazotoka...

Flatei Atimka Act, Arejea Ccm Kusaka Kura za Ushindi

ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Mbulu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Flatei Maasai ametangaza kurejea CCM akitokea ACT Wazalendo ambako aliteuliwa kugombea ubunge kupitia chama hicho huku akisisitiza kumuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu. Akizungumza wilayani Mbulu akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, Flatei alisema baada ya kuhama CCM alikutana na wazee ambao walimlea tangu akiwa mdogo wakimtaka kurejea ndani ya Chama. "Nilikutana na wazee wangu wa Chama ambao walinilea tangu nilipokuwa mtoto hadi leo, basi nikaona nikubali kurejea Chama Cha Mapinduzi. Kwa sisi watu wa Mbulu wakishakuja wazee wakikwambia kijana acha hivi na sisi tunaita wazee wa jani, likiwekwa jani la kijani mbele yao huwezi kuendelea tena. "Inabidi uwasikilize wazee wanasema nini, na mimi ninavyojua wazee hao ni wazee wangu na kwa sababu hawa wazee ni wa Chama wamekuja kwangu, zaidi ni kuwasik...

Waziri Mkuu Awataka Madereva wa Serikali Kufanyakazi Kwa Weledi

_Asisitiza wajiepushe na tabia zinazoharatisha maisha, mali na siri za Serikali_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa madereva wa Serikali wanawajibu wa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu ikiwemo ukaguzi wa gari kabla na baada ya safari, kujaza na kutunza kikamilifu taarifa za safari na matengenezo. Amewataka madereva na wasimamizi wahakikishe usalama wa vyombo vya usafiri, abiria, mizigo na nyaraka za Serikali pamoja na kutumia vifaa vya kisasa vya usalama, na kujiepusha na tabia zinazoweza kuhatarisha maisha, mali na siri za Serikali. Ameyasema hayo leo (Jumanne, Septemba 2, 2025) alipofungua Mkutano wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST), jijini Dodoma. Amesema chama hicho kimekuwa nguzo muhimu katika kuboresha huduma za udereva Serikalini na kuchangia maendeleo ya Taifa kwa ujumla. Pia, Waziri Mkuu amewahakikishia madereva hao kuwa Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili madereva ili kuendelea kuimarisha mazingira ...

TAKUKURU Rafiki Yatatua Kero 176 za Wananchi Tanga

Na Mwandishi Wetu,Tanga.  Programu ya TAKUKURU Rafiki imeendelea kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi wa Mkoa wa Tanga baada ya kutatua kero 176 kati ya 248 zilizobainika katika kata 21 zilizotembelewa. Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, Ramadhani Ndwatah, alisema kuwa programu hiyo inalenga kubaini kero zinazochochea vitendo vya rushwa katika sekta za afya, elimu, kilimo, maendeleo ya jamii, utawala na miundombinu. “Hili ni jukwaa muhimu la kuwasikiliza wananchi moja kwa moja na kupata mrejesho wa changamoto wanazokutana nazo kwenye maeneo yao ya huduma,” alisema Ndwatah na kuongeza kuwa kazi hiyo imekuwa ikitekelezwa kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika. Kwa mujibu wa Ndwatah, kati ya kero 248 zilizopokewa, kero 72 bado zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi na TAKUKURU inashirikiana na mamlaka husika kuhakikisha zinapata majibu stahiki kwa wakati. Aidha, alibainisha kuwa baadhi ya kero hizo zilihusiana na ucheleweshaji wa...

Mhandisi Mativila Afanya Ukaguzi Wa Miundombinu ya Barabara Wilayani Ukerewe

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila, amefanya ukaguzi wa miundombinu ya barabara zinazosimamiwa na Tarura katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, ambapo ameagiza wananchi kuhakikisha wanazitunza kwa kuzifanyia usafi ili zidumu kwa muda mrefu, badala ya kuzigeuza kama dampo la kutupitia takataka. Mhandisi Mativila amesema barabara hizo zikitunzwa vizuri zitachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi, ikiwemo kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji pamoja na kuongeza ajira kutokana na kupitika kipindi chote cha mwaka. Amesema serikali inaendelea kuimarisha mtandao wa barabara kwa kujenga barabara mpya na kuzifanyia matengenezo zilizopo, zikiwamo zilizopo chini ya wakala wa barabara za vijijini na mijini Naye meneja wa Tarura mkoa wa Mwanza Mhandisi Makori Kisare, akitoa taarifa ya matengenezo ya barabara za lami za RTC - Sungura yenye urefu wa Km 0.321 na barabara ya Pump House Km 0.299 katika mji wa Nansio, amesema barabara hiz...

Jwtz Kushiriki Zoezi La Pamoja La Sadc Nchini Zambia

  Na Mwandishi wetu,GMTV  MKUU wa majeshi ya ulinzi ya wananchi wa Tanzania jenerali Jacob John Mkunda,amekabidhi bendera ya Taifa kwa kikundi cha maafisa na Askari wa JWTZ kamandi ya jeshi la Anga kwa ajili ya kushiriki Mazoezi ya pamoja ya majeshi ya Anga kwa nchi za SADC ambayo yatafanyika nchini Zambia. Akizungumza wakati wa kukabidhi bendera hiyo ya Taifa kwa niamba ya mkuu huyo wa Majeshi ya ulinzi nchini,mkuu wa jeshi la Anga meja jenerali Shaban Baragash Mani,amesema maandalizi yote ya maafisa na Askari wa Jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania kamandi ya Anga yamekamilika kwa ajili ya kuanza safari na kushiriki mazoezi hayo muhimu. Amesema Tanzania imesaidia nchi za kusini mwa afrika katika kupigania uhuru wa nchi zao baada nchi kuwa huru hivi sasa kumeibuka majanga mengi ya kinadamu hivyo kutumia SADC lazima majeshi ya jumuiya hiyo kuhakikisha nchi wanachama wanakuwa salama. "Tanzania tutanufaika katika ushiriki wa zoezi hili, kwaza kupata zoefu namna ya kutoa msaa...