Na Mwandishi wetu,GMTV
MKUU wa majeshi ya ulinzi ya wananchi wa Tanzania jenerali Jacob John Mkunda,amekabidhi bendera ya Taifa kwa kikundi cha maafisa na Askari wa JWTZ kamandi ya jeshi la Anga kwa ajili ya kushiriki Mazoezi ya pamoja ya majeshi ya Anga kwa nchi za SADC ambayo yatafanyika nchini Zambia.
Akizungumza wakati wa kukabidhi bendera hiyo ya Taifa kwa niamba ya mkuu huyo wa Majeshi ya ulinzi nchini,mkuu wa jeshi la Anga meja jenerali Shaban Baragash Mani,amesema maandalizi yote ya maafisa na Askari wa Jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania kamandi ya Anga yamekamilika kwa ajili ya kuanza safari na kushiriki mazoezi hayo muhimu.
Amesema Tanzania imesaidia nchi za kusini mwa afrika katika kupigania uhuru wa nchi zao baada nchi kuwa huru hivi sasa kumeibuka majanga mengi ya kinadamu hivyo kutumia SADC lazima majeshi ya jumuiya hiyo kuhakikisha nchi wanachama wanakuwa salama.
"Tanzania tutanufaika katika ushiriki wa zoezi hili, kwaza kupata zoefu namna ya kutoa msaada ya kibinadamu kwa wenzetu wanapokuwa na majanga, na majeshi ya Anga yanasaidia kufika kwa haraka kwenye maeneo yaliyoathirika kwa kutoa msaada wa kibidamu pia ni sehemu ya kujiweka tayari wakati huu wa amani"alisema meja jenerali Shaban
Aidha amesema mazoezi hayo pia yatawawezesha kujifunza mbinu mpya za kukabiliana na majanga na kwamba washiriki wa Tanzania watatoa uzoefu wao kwa nchi washiriki juu kuokoa, kusaidia wakati wa majanga na maafa.
Kwa sababu hiyo hiyo amewataka maafisa na askari katika kikundi hicho,kuonesha uzalendo na nidhamu wakati wote wa ushiriki wa mazoezi hayo jambo ambalo litaipa Tanzania heshima kubwa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa oparesheni na mafunzo wa jeshi la Anga brigedia jenerali Zeno William Johnson Sikukuu,akizungumza katika hafla hiyo ambayo imefanyika katika viwanja vya kikosi cha Anga 603 KJ jijini Dar es salaam, amesema zoezi hilo linalojulikana kama SADC EX BLUE KUGWASHO 2025 ZAMBIA yanayaandaa majeshi hayo katika kukabiloana na majanga mbalimbali hasa wakati wa dharula.
Amesema ziezi hilo linatatarajia kufungukiwa Septemba 8 mwaka huu 2025 na kufungwa septemba 26 mwaka huu 2025 na kwamba katika zoezi hilo litagawanyika maeneo tofauti kŵa vikundi vitakavyogawanyika wakati wa zoezi hilo.
















