Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kawaida apokelewa Mwanza kuendeleza siku 10 za moto

  Mwenyekiti Wa UVCCM TAIFA Ndugu Mohamed Ali KAWAIDA Apokelewa Mkoani Mwanza Kuendelea Na Ziara Yake Ya Siku 10 Za Moto Mikoa Ya Kaskazini. Katika Ziara Hiyo Ndg KAWAIDA Ameongozana Na Makamu Mwenyekiti Wa UVCCM TAIFA Ndg Rehema SOMBI Pamoja Na Wajumbe Wengine Wa Kamati Ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa.

Azania Bank yadhamini na kushiriki mkutano wa Baraza la Viwanja vya Ndege (ACI Africa)

  Benki ya Azania imedhamini na kushiriki Mkutano wa 73 wa Baraza la kimataifa la Viwanja vya ndege (ACI Africa), unaofanyika katika hoteli ya Mount Meru jijini Arusha. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Uchukuzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) pia umehusisha Mikutano ya Kamati, Mikutano ya Kikanda na Maonesho ambapo wataalamu wa viwanja vya ndege nchini na Africa,watanufaika na kukuza ubora wakitaaluma ili kusaidia maendeleo endelevu sekta ya anga.

Waziri Mkuu atoa wito kwa Waandishi wa Habari nchini

  _▪️Awataka watumie akili mnemba kama nyenzo na si kikwazo cha uhuru wao_▪️ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Waandishi wa Habari nchini kutumia Akili Mnemba (Artificial Inteligence) kama nyenzo ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo na sio kikwazo cha uhuru wao. Amesema kuwa katika dunia ya sasa, vyombo vya habari vinakutana na changamoto mpya zinazotokana na maendeleo ya teknolojia, ambapo akili mnemba inachukua nafasi kubwa katika uzalishaji na usambazaji wa habari. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 29, 2025) katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ambayo kitaifa inafanyika Jijini Arusha kwenye Hoteli ya Gran Melia. Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuandaa sera maalum ya Akili Mnemba, ambayo itatoa mwongozo wa matumizi yake katika vyombo vya habari ili kuhakikisha kuwa teknolojia hiyo inaendana na misingi ya uhuru wa vyombo vya habari, uwazi, na uadilifu wa uandishi wa habari.   “Ni ukweli usiopingika ...

Majaliwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Aprili 29, 2025 ni mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari, inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Grand Melia jijini Arusha  Maadhimisho hayo yanalenga kubadilishana mawazo na kufanya majadiliano kuhusu fursa na changamoto katika sekta ya habari.

RC Batlida azindua mbio za magari zinazoitwa "𝗗𝗔𝗥 𝗧𝗧 𝗗𝗥𝗔𝗚 𝗥𝗔𝗖𝗘

  Na Mashaka Mhando, Muheza  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, amezindua mashindano ya mbio za magari maarufu kama Dar TT Drag Race katika eneo la Kigombe, Wilaya ya Muheza. . Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mashindano hayo, Balozi Dkt. Batilda ameipongeza timu ya Dar TT kwa kuichagua Tanga kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, akisema kuwa hatua hiyo itafungua fursa za kiuchumi kupitia sekta ya michezo. Balozi Dkt. Batilda amewakaribisha waratibu na wanamichezo wa mashindano ya aina hiyo kuendelea kuitumia barabara ya Tanga–Pangani kwa shughuli zao, akibainisha kuwa Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa barabara hiyo kama sehemu ya kukuza uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Tanga Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Zainabu Abdallah, amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kujitoa na kushirikiana kikamilifu katika kuendeleza michezo, hatua ambayo inaonesha dhamira ya dhati ya kumuunga mkono Rais Dkt. Samia...

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ametuletea Benki ya Ushirika vijijini nchini Tanzania

  Chigaitan mapinduzi vijijini  Katika mapinduzi ya kimaendeleo nchini Tanzania Mh.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewapelekea benk ya ushirika  watanzania vijijini. Anasema Dkt Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa benki ya Ushirika "Benki ya ushirika ni kichocheo cha maendeleo hasa ya kilimo vijijini" Kwa mtaji wa zaidi ya Bilion 50 benki ya Ushirika imezinduliwa haya ni mapinduzi ya kihistoria katika historia ya ushirika nchini Tanzania Kwa mujibu wa chigaitan mapinduzi vijijini.  Taifa lolote lenye ushirika na makampuni imara ndiyo nguzo kuu ya uchumi wa taifa. Leo nchini Tanzania waziri mkuu Kasimu Majaliwa,  Waziri kijana Hussein Bashe(Mb)  akishirikiana na  Abdulmajid Mussa Nsekela, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania wameongoza mapinduzi anayohubiri mwandishi mahiri wa mapinduzi vijijini nchini Tanzania CHIGAITAN Uchumi wa ushirika ni njia kuu ya mafanikio ya uchumi wa hasa watu wa vijijini nchini Tanzania.