Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania itaipambania Nafasi aliyoiacha Dkt. Ndugulile Kwa Nguvu zote

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaweka nguvu ile ile katika kupigania nafasi aliyoiacha Dk Faustine Ndugulile ili kuleta heshima kwa nchi. Mhe Rais Dkt Samia ametoa kauli hiyo Desemba 2, 2024 wakati akitoa salamu za pole kwenye shughuli maalumu ya kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Marehemu Dk Faustine Engelbert Ndugulile katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam. “ Dk Faustine katika safari yake hii ya mwisho ameweka heshima kubwa kwa nchi yetu kwa kupata nafasi ile, na niseme kwamba Mungu amechukua amana yake lakini kwetu sisi ni kwenda mbele, tutaingia tena kwenye ushindani wa nafasi ile, tutatafuta Mtanzania mwenye sifa zinazoweza kushindana na ulimwengu, tutaingia tena na tutweka nguvu ileile ili kuweka heshima ya nchi yetu” Amesema Dkt Samia. Dk Ndugulile kabla ya kifo chake aliteuliwa kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda y...

Waziri Mkuu ashiriki Kuaga Mwili wa Dkt. Ndugulile

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 02, 2024 ameshiriki katika tukio la kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile. Tukio hilo ambalo limefanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam limeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Naibu Waziri Mkuu ashiriki Misa na Kuaga Mwili wa Ndugulile

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Disemba 2, 2024 ameshiriki Misa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Dkt. Ndugulile na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Shirikisho la Mabunge Duniani (IPU).

Dkt. Biteko akiwasili Karimjee Kuaga Mwili wa Ndugulile

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Disemba 02, 2024 akisaini Kitabu cha Maombolezo kwenye msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Marehemu Dkt. Faustine Ndugulile. Dkt. Ndugulile alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 27, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.

Foundation for Disabilities Hope Yapata Ufadhili WA Kuimarisha Uongozi na Demokrasia

Na Hamida Ramadhan- Dodoma Foundation For Disabilities Hope,  (FDH)taasisi isiyokuwa ya kiserikali, imepata ufadhili wa shilingi milioni 40 kwa ajili ya mradi wa kuwawezesha watu wenye ulemavu katika masuala ya uongozi na kukuza demokrasia.  Ufadhili huo umetolewa na shirika la Abilis Foundation yenye ofisi zake nchini Tanzania, mkoani Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Foundation For Disabilities Hope, Michael Salali, alisema mradi huo unalenga kuwafikia watu 300 wenye ulemavu katika wilaya ya Kondoa. “Tunaimani mradi huu umekuja kwa wakati muafaka, hasa baada ya uchaguzi mdogo na kuelekea uchaguzi mkuu.  "Tunataka kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu kujitokeza kuchagua na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi bila kujihisi wanyonge,” alisema Salali. Hata hivyo Tasisi hiyo imeishukuru Abilis Foundation kwa kufanikisha mradi huo muhimu. Kwa upande wake Furaha William, Afisa Habari wa taasisi hiyo, alieleza kuwa mradi huo pia unalenga wanawake na was...

Waziri Kikwete aongoza Matembezi Kuchangia Wenye Ulemavu

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana,ajira na  wenye ulemavu mh Ridhwani Kikwete ameongoza Matembezi yanayojulikana kama Sunset Walk kuunga mkono taasisi inayosimamia haki za wenye Ualbino (TAS) na Lions Club. Matembezi hayo yamelenga kuchangia fedha kusaidia kupatikana kwa mahitaji muhimu kama Mafuta ya Ngozi, kofia kinga n.k .  Katika hotuba yeke Kikwete  amewakumbusha juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali ikiwemo mpango kazi wa kupambania haki za wenye Ulemavu wakiwemo wenye Ualbino utakao zinduliwa hivi karibuni..