Tanzania itaipambania Nafasi aliyoiacha Dkt. Ndugulile Kwa Nguvu zote

GEORGE MARATO TV
0

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaweka nguvu ile ile katika kupigania nafasi aliyoiacha Dk Faustine Ndugulile ili kuleta heshima kwa nchi.

Mhe Rais Dkt Samia ametoa kauli hiyo Desemba 2, 2024 wakati akitoa salamu za pole kwenye shughuli maalumu ya kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Marehemu Dk Faustine Engelbert Ndugulile katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.



“ Dk Faustine katika safari yake hii ya mwisho ameweka heshima kubwa kwa nchi yetu kwa kupata nafasi ile, na niseme kwamba Mungu amechukua amana yake lakini kwetu sisi ni kwenda mbele, tutaingia tena kwenye ushindani wa nafasi ile, tutatafuta Mtanzania mwenye sifa zinazoweza kushindana na ulimwengu, tutaingia tena na tutweka nguvu ileile ili kuweka heshima ya nchi yetu” Amesema Dkt Samia.

Dk Ndugulile kabla ya kifo chake aliteuliwa kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika baada ya kushinda uchaguzi wa kuwania nafasi hiyo.
















Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top