Na Mwandishi Wetu BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kwa miongo minne imefanikiwa kutoa vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA), kwa miradi 35,000 hatua iliyowezesha uwekezaji kufanyika kwa uwajibikaji mkubwa zaidi. Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo, Dk Immaculate Semesi, wakati akizungumzia miaka 40 ya NEMC na safari ya Tanzania kuelekea mustakabali wa kijani na maendeleo endelevu. Dk Semesi alisema hiyo si takwimu tu bali ni ni ushahidi wa namna Tanzania ilivyofanikiwa kuoanisha ukuaji wa uchumi na ulinzi wa mazingira. Alisema katika sekta ya viwanda na biashara, utoaji wa vibali zaidi ya 28,000 umeimarisha uzingatiaji wa viwango vya mazingira, hivyo kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya kimataifa. Aidha, alisema juhudi za kudhibiti uchafuzi wa mazingira zimeokoa taifa gharama kubwa ambazo zingetumika kurekebisha madhara ya kimazingira na kiafya. “Uwekezaji katika maarifa nao haujaachwa nyuma kwani kupitia mafun...
Marato tv - Sauti ya Jamii