Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

NEMC yatoa vyeti vya EIA kwa miradi 35,000 tangu kuanzishwa

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kwa miongo minne imefanikiwa kutoa vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA), kwa miradi 35,000 hatua iliyowezesha uwekezaji kufanyika kwa uwajibikaji mkubwa zaidi. Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo, Dk Immaculate Semesi, wakati akizungumzia miaka 40 ya NEMC na safari ya Tanzania kuelekea mustakabali wa kijani na maendeleo endelevu. Dk Semesi alisema hiyo si takwimu tu bali ni ni ushahidi wa namna Tanzania ilivyofanikiwa kuoanisha ukuaji wa uchumi na ulinzi wa mazingira. Alisema katika sekta ya viwanda na biashara, utoaji wa vibali zaidi ya 28,000 umeimarisha uzingatiaji wa viwango vya mazingira, hivyo kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya kimataifa. Aidha, alisema juhudi za kudhibiti uchafuzi wa mazingira zimeokoa taifa gharama kubwa ambazo zingetumika kurekebisha madhara ya kimazingira na kiafya. “Uwekezaji katika maarifa nao haujaachwa nyuma kwani kupitia mafun...

Waziri wa Fedha na Mkuu wa Mkoa Dodoma wajadili fursa za uwekezaji mkoani Dodoma

Na Benny Mwaipaja, Dodoma Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Mkoa wa Dodoma una fursa nyingi za kiuchumi na kijamii katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, biashara, utalii na madini ambazo zikiendelezwa na kuchangamkiwa ipasavyo zitakuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na watu wake. Mhe. Balozi Omar amesema hayo alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kujitambulisha, baada ya hivi karibuni kuteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa Waziri wa Fedha. Alisema kuwa Mkoa wa Dodoma uko katikati ya nchi na unaweza kutumika ipasavyo kama kitovu ama kituo cha biashara kwa kuunganika na mikoa mingine kimkakati ikiwemo bandari kavu kwa ajili ya kuhifadhi na kusafirisha makontena na bidhaa nyingine Kwenda maeneo mengine ya ndani na nje ya nchi. “Lakini pia tuna fursa kubwa ya kilimo ambayo imeajiri watanzania wengi zaidi, mazao tofauti, fursa ya...

Waziri Mkuu Awasili Mkoani Iringa,Kuelekea Njombe

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Iringa, ambapo anatarajiwa kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yatakayofanyika mkoani Njombe, Mei 1, 2026.

Acheni Kutangaza Watu, Tangazeni Nchi - Makonda

*Na Immaculate Makilika - MAELEZO* Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda amewataka wadau wa sekta ya habari  kubadili ajenda ya kutangaza watu badala yake watangaze fursa za uchumi zilizopo nchini. Ametoa rai hiyo leo Aprili 30, 2026 katika Siku ya Tatu ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani iliyofanyika jijini Arusha. “ Tuache ajenda ya kutangaza watu, tuitangaze nchi yetu. Tubadilishe mkakati kutoka ajenda ya kusifia watu, tuambieni fursa za uchumi zilizopo,” amesema Waziri Makonda Ameongeza kuwa waandishi wa habari waache kasumba ya kuwaandika vizuri wala rushwa na watu wasio na sifa njema katika jamii, badala yake wafanye kazi zao kwa maslahi ya Taifa.  Ametolea mfano kuwa hakuna idadi ya kutosha ya waandishi wanaoandika kuhusu sekta ya utalii au kilimo kama wanaoandika kuhusu masula ya siasa. Amezungumzia kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na kuwaasa waandishi wa habari kushiriki kikamilifu ili kufikia malengo yaliyowek...

Mapinduzi ya Kidijitali:Intanet Yafikia asilimia 94,Serikali yaongeza ngugu ya Tehama

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki, amesema Tanzania inapiga hatua kubwa katika safari ya kidijitali, baada ya huduma ya intaneti ya kasi kufikia asilimia 94 ya maeneo ya makazi, huku watumiaji wakifikia asilimia 85.3 ya wananchi. Akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma leo Aprili 30, 2026, Kairuki ameeleza kuwa mafanikio hayo yanatokana na uwekezaji mkubwa wa Serikali katika miundombinu ya mawasiliano, hususan kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. “Tumeongeza uwezo wa Mkongo wa Taifa kutoka 200Gbps hadi kufikia kati ya 400Gbps na 2,000Gbps kwenye njia kuu, huku maunganisho ya mipakani yakiongezwa hadi 800Gbps ili kuboresha kasi na upatikanaji wa huduma za mtandao,” amesema Kairuki. Katika kuimarisha zaidi sekta ya TEHAMA, Serikali imetenga shilingi bilioni 12.16 kwa ajili ya Mradi wa Tanzania ya Kidijitali, hatua inayolenga kuharakisha mageuzi ya teknolojia na kukuza uchumi wa kidijitali nchini. Mradi huo una...

Waziri Mkuu Wateta na Spika wa Bunge wakiwa Uwanja wa ndege

   Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu walipokutana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakielekea Dodoma, leo tarehe 30 Aprili, 2026.