Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Aweka Jiwe la Msingi Mradi wa Umwagiliaji Bonde la Eyasi

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 6, 2026 ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa skimu za umwagiliaji katika Bonde la Eyasi, lililopo Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha. Mradi huo unaotekelezwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji utagharimu shilingi bilioni 38.4. Hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba mwaka huu. Kukamilika kwa mradi huo utanufaisha zaidi ya wakulima 2,500 kutoka skimu za Mang’ola Barazani, Maleckchand, Laghangareri, Mbuga Nyekundu, Jobaji na Dumbechand, zenye zaidi ya hekta 5,000. Aidha, utekelezaji wa mradi huo utasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa upotevu wa maji unaotokea katika mifereji ya asili, hatua itakayoongeza ufanisi wa matumizi ya maji na kuimarisha uzalishaji wa mazao katika eneo hilo.

Wananchi Waombwa Kushiriki Kikamilifu Kulinda Vyanzo Vya Maji

 DODOMA. MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Maji Bonde la ziwa Victoria Dkt. Renatus James Shinhu, amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda vyanzo vya maji, kutunza miundombinu iliyojengwa, kuzuia uchafuzi wa mazingira na kutumia rasilimali za maji kwa uangalifu kwa kuzingatia sheria zilizopo. Amesa ulinzi wa rasilimali za maji haupaswi kuwa jukumu la taasisi za serikali pekee, bali unahitaji ushiriki wa wananchi wote katika kuhifadhi mito, maziwa na vyanzo vingine vya maji. Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dodoma wakatika akieleza Mafanikio yaliyopatikana katika siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dk. Renatus Shinhu ameeleza kuwa kila mwananchi anapaswa kutambua kuwa maji ni maisha na ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya jamii, hivyo kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji ni jukumu la kila mmoja ili kuhakikisha rasilimali hiyo inaendelea kuwepo kwa matumizi endelevu. "Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria itaendelea kusimamia rasilimali hizi muhimu kwa ...

Ccm na Frelimo Kuimarisha Ushirikiano wa Kiuchumi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO, (Msumbiji), Ndugu Chakil Felizardo Passadas Aboobacar, ambaye ameanza ziara rasmi ya kikazi kwa siku mbili nchini.  Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo tarehe 6 Machi 2026, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar Es Salaam, vyama hivyo viwili ambavyo vina urafiki na udugu wa kihistoria, vimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya pande hizo mbili, hasa kushirikiana kiuchumi.

Dkt. Mwigulu Kufanya Ziara Karatu na Monduli

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja mkoani Arusha katika Wilaya za Karatu na Monduli. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anategemea kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa  skimu za umwagiliaji katika Bonde la Eyasi, lililopo Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha. Pia, Mheshimwa Dkt. Mwigulu atafanya mikutano ya hadhara Karatu mjini pamoja na Mto wa Mbu Wilayani Monduli

Wadau wa Maendeleo na Vyama Vya Siasa Mkoani Mara Wampongeza Rais Samia Kwa Kutekeleza Ahadi Zake

Na Mwandishi wetu Jovina Massano ;Musoma. WADAU wa Maendeleo na vyama vya kisiasa mkoani Mara wampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa akiomba kura kwa  wananchi. Pongezi hizo zimetolewa katika kikao Cha Baraza la Ushauri la  mkoa(RCC) na wadau wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa  mara baada ya kupokea taarifa ya usajili wa Kaya zisizo na uwezo katika mpango wa Bima ya Afya kwa wote uliozinduliwa  Januari,23,2026. Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani hapa Kuhunga Patrick Msambichaka amesema katika mkoa huu Serikali tayari imewaripia wasio na uwezo wapatao 62,444 mpaka sasa wamekwisha fanya uhakiki na kusajili kaya zisizo na uwezo na kuwafikia wahitaji 17,205 katika kata zote za mkoa  sawa na asilimia 27.6. Katibu wa Jimbo wa chama Cha ACT Wazalendo Musoma mjini Abdalah Songe amesema Serikali imekuwa sikivu kwa wananchi wake mchakato huo ni mzuri na una manufaa kwa w...

Mpasuko Mkubwa Chadema, Zanzibar Yadai Haki

 Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kwa upande wa Zanzibar, Mh. Said Issa Mohammed amesema Kuwa lengo la kufungua shauri la mgawanyo wa mali za chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sikutaka kufutwa kwa chama kama wanachama wengine wanavyo dhania. Hayo amebainisha mapema hii leo, Machi 5, 2026, jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kutoa ufafanuzi wa mambo kadha kuhusu chanzo cha kufungua shauri la mgawanyo wa mali za chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), ambapo amesema chama cha hiko katika mwaka 2015-25 kilifanikiwa kupokea ruzuku ya kiasi kisichopungua cha shilingi milioni 117 kama pesa ya kuendeshe chama ambapo kwa upande wa Zanzibar kiasi cha milioni 2 tu ndicho kilipatiwa ambacho hakiendani na ghalama zauendeshaji wa chama kwa upande wa Zanzibar. Aidha mwenyekiti huyo mstaafu amesema kuwa hadi kufikia sasa chama cha (CHADEMA) kimehama katika jengo lake la makao mak...