Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kwa upande wa Zanzibar, Mh. Said Issa Mohammed amesema Kuwa lengo la kufungua shauri la mgawanyo wa mali za chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sikutaka kufutwa kwa chama kama wanachama wengine wanavyo dhania.
Hayo amebainisha mapema hii leo, Machi 5, 2026, jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kutoa ufafanuzi wa mambo kadha kuhusu chanzo cha kufungua shauri la mgawanyo wa mali za chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), ambapo amesema chama cha hiko katika mwaka 2015-25 kilifanikiwa kupokea ruzuku ya kiasi kisichopungua cha shilingi milioni 117 kama pesa ya kuendeshe chama ambapo kwa upande wa Zanzibar kiasi cha milioni 2 tu ndicho kilipatiwa ambacho hakiendani na ghalama zauendeshaji wa chama kwa upande wa Zanzibar.
Aidha mwenyekiti huyo mstaafu amesema kuwa hadi kufikia sasa chama cha (CHADEMA) kimehama katika jengo lake la makao makuu madogo mkwajuni Zanzibar kufuatia deni la pango la kiasi cha shilingi milioni 12 hali ambayo si nzuri kwa ustawi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwa upande wa Zanzibar huku chama kikishindwa kutoa hata gari moja kwa upande huwo.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesikitishwa na baadhi ya viongozi wakuu wa chama kutojali imani za kidini kwa wananchama wengine hali ambayo inaweza kusababisha mpasuko na sintofahamu kwa baadhi ya wanachama wa chama hiko cha CHADEMA.
Hata hivyo Makamu huyo amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya taarifa kutoka sehemu mbalimbali zikimuhusisha na kutumika na baadhi ya watu katika kukishitaki chama hiko jambo ambalo amekanusha kuhusika na vitendo hivyo kupitia kesi hiyo.
Sambamba na hilo Said Issa amesema kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa katika baadhi ya nafasi katika chama hicho huku akitolra mfano nafasi ya Mkurugenzi wa mawasiliano ya Chama hiko upande wa Zanzibar hali ambayo si nzuri kwa ustawi bora wa chama hicho.
Kupitia mkutano huwo, Makamu Mwenyekiti huyo amesema hali halisi ya chama kwasasa si nzuri hivyo jitihadq zinahitqjika katika kujenga ustawi bora wa chama kiujumlq katika upande wa Zanzibar.





