Wadau wa Maendeleo na Vyama Vya Siasa Mkoani Mara Wampongeza Rais Samia Kwa Kutekeleza Ahadi Zake

GEORGE MARATO TV
0


Na Mwandishi wetu Jovina Massano ;Musoma.

WADAU wa Maendeleo na vyama vya kisiasa mkoani Mara wampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa akiomba kura kwa  wananchi.

Pongezi hizo zimetolewa katika kikao Cha Baraza la Ushauri la  mkoa(RCC) na wadau wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa  mara baada ya kupokea taarifa ya usajili wa Kaya zisizo na uwezo katika mpango wa Bima ya Afya kwa wote uliozinduliwa  Januari,23,2026.


Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani hapa Kuhunga Patrick Msambichaka amesema katika mkoa huu Serikali tayari imewaripia wasio na uwezo wapatao 62,444 mpaka sasa wamekwisha fanya uhakiki na kusajili kaya zisizo na uwezo na kuwafikia wahitaji 17,205 katika kata zote za mkoa  sawa na asilimia 27.6.

Katibu wa Jimbo wa chama Cha ACT Wazalendo Musoma mjini Abdalah Songe amesema Serikali imekuwa sikivu kwa wananchi wake mchakato huo ni mzuri na una manufaa kwa wananchi hasa wasio na uwezo utekelezaji huu utaendana na kiu ya wananchi.

" Lakini pia ameiomba Serikali kupitia mchakato wake huu upelekwe kwenye Serikali za mitaa kwa kuwa ndio wanaowatambua wananchi wasio na uwezo bila upendeleo", amesema Abdalah.

Ameongeza kuwa ujio wa Bima hii ya Afya kwa wote utakuwa mwarobaini kwa watanzania kwa maslahi ya Taifa na kupunguza umaskini kwa kuokoa ghalama wakati wa matibabu.

Aidha amewaomba wananchi kuupokea mchakato huu ulio na unafuu kwa kujiunga kwa wingi bila kusita ili kuokoa vipato vyao.

Katika kuendeleza mapinduzi ya sekta ya Afya nchini Wizara ya Afya chini ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na  Dkt. Samia Suluhu Hassan ilioma umuhimu wa kuimarisha upatikanaji na ubora wa huduma za afya katika ngazi zote na kuja na mpango utakaoweza kuinufaisha jamii kwa kupunguza ghalama zisizo za lazima wa Bima ya Afya kwa wote kuondoa adha wakati wa kupata matibabu.

Katika Baraza hilo ambalo Mwenyekiti wake ni mkuu wa mkoa huu Kanali Evans Mtambi pia imetolewa taarifa ya miradi ya maendeleo itakayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/2027 katika sekta za maji na umeme imetolewa,ambapo imepitisha makadirio  ya bajeti ya Billioni 448,996,863,000 kwa ajili ya Sekretarieti ya mkoa wa Mara na Mamlaka za Serikali za mitaa.

Sambamba na hayo wadau wameweza kumpongeza Dkt. Samia kwa kuweza kutimiza ahadi zake na kuleta matumaini kwa wananchi na Serikali kwa ujumla.

Aidha Mwenyekiti  Kanali Evans Mtambi amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata Bima ya Afya kwa wote lengo kuwa na uhakika wa afya zao pindi wanapougua na kupunguza ghalama zisizo za lazima.


         

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top