Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Miradi ya CSR Ya Migodi Yawanufaisha Wananchi Simiyu

📍Simiyu Serikali imesema itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) inayotekelezwa na kampuni za uchimbaji madini nchini, ili kuhakikisha wananchi wanaoishi jirani na migodi wananufaika moja kwa moja na shughuli za uchimbaji madini. Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Simiyu, Mayigi Makolobela, alisema hayo hivi karibuni alipokagua utekelezaji wa miradi ya CSR inayofanywa na kampuni za uchimbaji madini katika mkoa huo, akibainisha kuwa miradi hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya na miundombinu ya umeme. “Serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta ya madini katika kukuza uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya wananchi. Ndiyo maana tunasisitiza kampuni zote za uchimbaji, zikiwemo zinazomilikiwa na wachimbaji wadogo, kutekeleza wajibu wao wa kijamii kupitia miradi ya CSR ili jamii inayoishi jirani na migodi inufaike moja kwa moja na rasilimali hizo,” alisema Makolobela. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ...

Mbunge Mavunde Aanzisha Ujenzi wa Zahanati Mtaa wa Maseya-Hombolo Makulu

▪️Wananchi wampongeza kwa kuanza kutimiza ahadi yake ▪️Aapa kukamilisha ujenzi kwa wakati ▪️Wananchi wamshukuru Rais Samia kwa visima vya umwagiliaji na Umeme Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde leo ameshiriki na mamia ya wananchi wa Mtaa wa Maseya-Kata ya Hombolo Makulu kuanzisha ujenzi wa Zahanati katika mtaa huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025. “Nawashukuru wananchi wa Maseya kwa kumchagua Rais Samia,mimi na Diwani wa kata yetu kwa kura nyingi sana kwenye uchaguzi mkuu uliomalizika. Kazi yetu sasa ni kufanya kazi na kutatua changamoto za wananchi,nawapongeza kwa kuitikia wito wa ujenzi wa zahanati yetu ambayo itasaidia kusogeza karibu huduma ya Afya kwa wananchi wetu. Nitakabidhi matofali 2000 na saruji mifuko 100 ili kulifikisha juu jengo letu mpaka hatua ya upauaji,ni imani yangu kwamba serikali yetu sikivu itatuunga mkono ukamilishaji wa zahanati hii”Alisema Mavunde Akitoa salamu za wananchi,Mwenyekiti wa Mtaa wa Maseya Ndg. Alexande...

ZAIDI YA WANANCHI 1,5000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJIKO BANIFU WILAYANI BABATI

📌 *Majiko banifu 1,582 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku* .   📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200* . 📍 *BABATI*  Mkuu wa Wilaya ya wa Babati, Mheshimiwa Emmanuela Kaganda, leo Novemba 12, 2025 kwa niaba ya wakazi wa wilaya ya babati amezindua mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku.   Uzinduzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga akiwataka wakuu wa wilaya wote wa mkoa wa manyara kuzindua na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika wilaya zao. Uzinduzi umefanyika katika kata ya Magugu wilayani babati, ambapo jumla ya majiko banifu  1,582 yatauzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200 ambayo ni sawa na aslimia 80 ya ruzuku ya TZS 56,000 ambayo ni bei ya awali ya jiko. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Kaganda amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa k...

Wachimbaji Wadogo wa Madini Simiyu Wapaza Sauti: “Tunaweza Tukipewa Umeme na Mikopo

Simiyu WACHIMBAJI Wadogo wa Madini wa Mkoa wa Simiyu wameiomba Serikali pamoja na taasisi za kifedha kuwaunga mkono kwa kuwapatia umeme wa kudumu na mikopo yenye masharti nafuu, wakisema changamoto hizo zimekuwa kikwazo kikubwa katika kuongeza uzalishaji wa madini, hususan dhahabu. Mmoja wa wachimbaji wanawake kupitia Chama cha Wachimba Madini Wanawake Tanzania (TAWOMA) mkoani humo, Anisia Japhet, amesema wamekuwa wakitumia gharama kubwa kuendesha mitambo kutokana na kutegemea nishati ya dizeli. “Tunatumia dizeli ambayo ni ghali. Lita 80 zinamalizika ndani ya saa 24. Tungepata umeme wa kudumu, tungepunguza gharama na kuongeza tija,” amesema Anisia. Ameongeza kuwa uchimbaji si kazi ya wanaume pekee bali ni fursa yenye manufaa makubwa kwa wanawake wanaojituma. “Nikiwa mwanamke, nimefanikiwa kusomesha watoto na kuendesha maisha yangu kupitia uchimbaji. Kila mwezi tunapata wastani wa viroba 100 vya mawe, na kila kiroba kinaweza kutoa gramu moja au zaidi za dhahabu,” ameongeza. Kwa upande w...

Ulinzi wa Msitu wa Mgori Kuimarika

TFS kuongeza askari, vifaa na kujenga kituo cha walinzi Pohama Na Mwandishi Wetu, Singida Ulinzi wa Msitu wa Hifadhi wa Mgori mkoani Singida unatarajiwa kuimarika baada ya Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo, kutangaza mpango wa kuongeza askari, kupeleka vifaa vya kisasa vya ulinzi na kuanzisha ujenzi wa Ranger Post katika kijiji cha Pohama. Profesa Silayo alitoa ahadi hiyo leo Jumanne, Novemba 11, 2025,  wakati wa kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Singida, kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mhe. Godwin Gondwe, kwa lengo la kujadili mikakati ya kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa Msitu wa Mgori. Msitu huo, ambao ni miongoni mwa hifadhi muhimu nchini, umekuwa ukikabiliwa na changamoto za uchomaji moto, ukataji miti holela na uvamizi unaoathiri juhudi za Serikali katika kulinda rasilimali za misitu. Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Gondwe alisisitiza umuhimu wa uhifadhi shirikishi, akipendek...

VERONICA MGETA AHIMIZA MSHIKAMANO WA KITAIFA

Alieyekua mgombea ubunge wa jimbo la Ilemela Veronica Calist Mgeta katika hutuba yake mbele ya wandishi wa habari amesema kufuatia uungwaji mkono alioupata wakati wa uchaguzi mkuu oktoba 29 Jimbo la Ilemela ni dhahiri kuwa anadeni kubwa kwa wanachi. “Imani yangu kwa wapiga kura ni kubwa namna mlivyojitokeza hakika ungwaji mkono huu sikua nautegemea hivi mmenipa heshima kubwa maishani mwangu najiona mwenye deni sina cha kuwalipa ila mungu pekee ndie anaweza kuwatosheleza alisema mgeta” Mgeta amesema kampeni zilizofanyika kata 19 za jimbo la ilemela zimeshuhudiwa   na wananchi  waliojitokeza kwa wingi katika mikutano yetu ya kampeni ili kutusikiliza sera mikakati ya kuwaleta maendeleo wananchi endapo CHAUMMA ingeshinda . Veronica alisema shukrani pekee hazitoshi ila ataendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kuyafikia maendeleo endelevu na kujenga uchumi wa jamii ya wana Ilemela wote kwa kuzingatia misingi ya utu na uzalendo. Aidha Veronica Mgeta amesema Uch...